Friday, January 02, 2009

masikini chadema

VIONGOZI na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana waliachwa wakitafakari cha kufanya baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutupilia mbali rufaa ya mgombea wao kupinga kuenguliwa kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa Mbeya Vijijini.
Mgombea wa Chadema, Sambwee Shitambala alienguliwa na Tume ya Uchaguzi ya Mbeya Vijijini baada ya vyama vya CCM na CUF kuwasilisha pingamizi, vikidai kuwa alikiuka Sheria ya Uchaguzi kwa kuapa kwa wakili badala ya kwa hakimu. Mgombea huyo hakukubaliana na uamuzi huo na kukata rufaa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Lakini jana, mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Lewis Makame aliwaambia waandishi wa habari kwenye hoteli ya Mount Livingstone kuwa baada ya kutafakari mambo makuu manne, tume yake imetupilia mbali rufaa hiyo.
"Siwezi kueleza chochote kwa sasa kwa sababu tunahitaji kufanya consultations (mashauriano)," alisema mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alipotakiwa kuzungumzia hatua inayofuata baada ya Jaji Makame kutangaza uamuzi huo, habari hizi katupasha Brandy Nelson kutoka Mbeya.



No comments:

NAIBU WAZIRI WA FEDHA AMWAKILISHA WAZIRI WA FEDHA KATIKA KONGAMANO LA 16 LA MWAKA LA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI – ARUSHA

Naibu Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Mhandisi Mshamu Ali Munde, amemwakilisha Waziri wa Fedha katika ufunguzi wa Kongamano la 16 la Mwaka la Wa...