Thursday, January 22, 2009

ATCL yaanza kazi bila Sh5 bn



SHIRIKA la Ndege Tanzania (ATCL) linaanza tena kutoa huduma za usafiri leo huku likiwa halijapatiwa Sh5.1 bilioni lilizoomba ili liweze kuendesha shughuli zake kikamilifu.

Kuanza kwa huduma hizo leo kunatokana na agizo la Rais Jakaya Kikwete alilolitoa Ijumaa iliyopita la kuamuru menejimenti ya ATCL, Wizara ya Miundombinu pamoja na Hazina kuhakikisha shirika hilo linarudisha huduma zake haraka iwezekanavyo.

Utekelezaji wa agizo hilo umekuja siku saba tangu lilipotoplewa Ikulu na rais mbele ya viongozi wa Wizara ya Miundombinu baada ya menejimenti ya ATCL kumueleza sababu zilizochangia kufungiwa kutoa huduma na Mamlaka ya Udhibiti wa Safari za Anga (TCAA) Desemba 8, mwaka jana.

Licha ya ATCL kurejeshewa leseni yake siku 23 baadaye na serikali kulipatia Sh2.5 bilioni, shirika hilo lilishindwa kuanza tena safari zake kutokana na kukabiliwa na mzigo wa madeni. Lilikuwa likihitaji Sh7.1 bilioni ili liweze kurejkesha huduma zake kama ilivyokuwa awali.

No comments: