pichani ni Mwanajeshi mmoja ambaye hakujulikana ni wa kikosi gari akiwa anasambaza watu waliokuwa wamefurika katika eneo la ajali na hivyo kuzuwia uokowaji, na awali polisi walikuwa wakipata taabu kufukuza watu hao.
Kaimu Kamanda wa polisi mkoani Arusha, Rober Boaz akiwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru katika eneo la ajali hiyo jana.
pichani ni gari aina ya Scania likijitahidi kulivuta basi dogo la abiria mara baada ya ajali hiyo ili kuendelea na ukowaji watu jana jioni.
picha zote na mussa juma
WATU 15 wamefariki dunia na wengine 12 wamejeruhiwa vibaya baada ya magari matano kupata ajali katika daraja la mto Nduruma wilayani Arumeru jana mchana na moja kutumbukia ndani ya mto.
Tukio hilo la aina yake, ambalo lilisababisha kufungwa kwa barabara ya Arusha- Moshi kuanzia majira mchana hadi saa 12 jioni lilisababishwa na magari hayo kukutana katika daraja hilo jembamba na gari moja ya abiria kukosa breki.
Katika ajali mbaya iliyoyahusisha magari matano na kuthibitishwa na Kaimu kamanda wa polisi mkoani Arusha, Robert Boaz chanzo kamili cha ajali kilikuwa bado hakijajulikana licha ya kuelezwa ni gari dogo la abiria kukosa breki na kuanza kuparamia mengine.
Magari ambayo yalihusika katika ajali hiyo, ni basi la abiria aina ya Fuso la kampuni Lim Safari lililokuwa linatoka Arusha kwenda Moshi.
Jingine ni Land Rover lililokuwa linatoka Tengeru kuja Arusha, gari dogo la abiria lililokuwa linatoka Arusha kwenda Moshi, Scania lililokuwa na shehena ya chupa za soda. Habari na Mussa Juma wa Arusha
Comments