Tuesday, December 04, 2012

KATIBU Mpya wa NEC, Oganaizesheni CCM, Dk. Muhamed Seif Khatib Akabidhiwa Rasmi Ofisi Leo

KATIBU wa NEC, Oganaizesheni Dk. Muhamed Seif Khatib (kushoto) akikabidhiwa ofisi na aliyekuwa akishika wadhifa huo kabla ya mabadiliko ya Sekretarieti ya CCM yaliyofanyika hivi karibuni, Asha Abdalaah Juma, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika, leo Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Kushoto Ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Uchaguzi kilichopo Idara ya Oganaizesheni, Matson Chizi. 
KATIBU wa NEC, Oganaizesheni Dk. Muhamed Seif Khatib (kushoto)Wakisaini hati za makabidhiano ya Ofisi na aliyekuwa akishika wadhifa huo kabla ya mabadiliko ya Sekretarieti ya CCM yaliyofanyika hivi karibuni, Asha Abdalaah Juma, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika, leo Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Kushoto Ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Uchaguzi kilichopo Idara ya Oganaizesheni, Matson Chizi.Picha na Bashir Nkoromo

KUSAGA AMWALIKA MWANAMZIKI JB MPIANA CHAKULA CHA USIKU

Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga akiwakaribisha wageni wake, akiwemo mwanamuziki nyota wa dansi ndani ya kundi la Wenge BCBG,kutoka nchini DRC-Congo, JB Mpiana (pichani kati) kwenye hafla fupi ya chakula cha usiku iliyofanyika kwenye kiota cha maraha cha Escape 2, kilichopo Kunduchi jijini Dar, hafla hiyo pia ni sehemu ya muendelezo wa shamra shamra za maadhimisho ya miaka 13 ya Clouds FM tangu kuanzishwa kwake hapa nchini.
 Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga akiwakaribisha wageni wake na kuzungumza nao machache na kuhakikisha wanapatiwa chochote kitu.
 Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akimtambulisha mke wake Johayna Kusaga  (ambaye ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Prime Time Promotions Ltd) kwa Mwanamuzik JB Mpiana na kwa wageni wengine waliofika kwenye hafla hiyo ya chakula cha pamoja.
 Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akimkaribisha mgeni wake JB Mpiana kwenye chakula
 Pichani ni baadhi ya Washiriki wa shindano la Miss East Afrika  2012 ambao pia walialikwa kwenye chakula cha pamoja ndani ya kiota cha maraha cha Escape 2,kilichopo Kunduchi jijini dar.
 Washiriki wa shindano la Miss East Afrika wakiwa katika picha ya pamoja
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Cassim akitumbuiza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali 
 Boniventure Kilosa a.k.a Dj Venture alikamata mashine na kuangusha ngoma kali zikiwemo za Kinaija,abazo wageni wengi walionekana kuburudishwa nazo vilivyo.
 Washiriki wa shindano la Miss East Afrika 2012 wakijiachia vilivyo kwa mikato ya ngoma iliokuwa ikiangushwa na Dj Venture.
 Joseph Kusaga a.k.a Boss JOe akizungumza na baadhi ya wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Ay na Mwana FA ndani ya hafla fupi ya chakula cha usiku kulichoandaliwa kwa ajili ya wageni.
 Wadau nao walikuwepo.Mdau wa MJ FM pamoja na Andrew Kusaga wakishoo love.
Wafanyakazi mbalimbali kutoka Clouds Media Group walikuwepo pia
Kuserebuka kama hivi pia kulikuwepo  .
 Mtangazaji wa Clouds TV,Ben Kinyaiya akifanya mahojiano mafupi na mwanamuziki mkongwe wa dansi,Ndandaa Kossovo.
 Dj Venture na mshkaji wake wakivuta pumzi.
 Mmoja wa Wakurugenzi wa Prime Time promotios,pichani kulia Godfrey Kusaga akibadilishana mawazo na Mtangazaji mahiri wa kipindi cha Jahazi cha Clouds FM,Ephrahim Kibonde huku wakiangusha moja moja.
 Mazungumzo ya hapa na pale pia yalikuwepo.
Pichani shoto ni Dj Bon Love,Balozi,Godliva pamoja na Ephraim Kibonde wakishoo love.

Monday, December 03, 2012

SHY ROSE BANJI AKUTANA NA KIONGOZI MTUKUFU AGA KHAN


Kiongozi Mtukufu Aga Khan ambaye ndiye Mwenyekiti wa Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN) na Kiongozi wa Waislamu wa Ismailia akizungumza mawili matatu ya kimaendeleo na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania Mh. Shy-Rose Bhanji wakati wa ufunguzi wa Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki mkoni Arusha. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Masuala ya Kidiplomasia ya AKDN Dkt. Shafik Sachedina. ( Picha zote kwa Hisani ya Ikulu).

JENGO LA MAKUMBUSHO BEIT AL JAIB ZANZIBAR LAPOROMOKA

Gari ndogo yenye nambari za usajili Z 897 DF ikionekana kuvurugika kabisa baada ya kifusi cha dari ya jengo la Makumbusho ya Taifa la Beit al ajaib kuidondokea kufuatia mvua za vuli zinazoendelea kunyesha Zanzibar.

Jengo la Beit Al- Ajaib lililojengwa na Utawala wa Kijerumani Mwaka 1870 likiwa na umri wa karibu miaka 142 hutegemewa sana katika Sekta ya Utalii ndani ya mwambao wa Afrika Mashariki pamoja na wataalamu na wanafunzi wa kigeni wanaokuja kufanya utafiti hapa Nchini.

JOSEPH SENGA AUAGA UKAPERA



Mpiga Picha Mkuu wa gazeti la Tanzania Daima, Joseph Senga leo Desemba 1, 2012 ameamua kuachana na Ukapera rasmi na kufunga pingu za maisha na mke wake, Fridah Mockray. Pichani ni wanandoa hao wakiwa Kanisani wakati wa ibada ya ndoa takatifu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Sinza jijini Dar es Salaam jioni ya jana.
Matron akisaini cheti
Maharusi wakiwa katika picha ya pamoja na wasimamizi wao. 
 Maharusi wakisaini hati za ndoa.
Joseph Senga akisaini cheti.
Maharusi wakikabidhiwa Shahada zao za ndoa.
 Mpiga Picha Mkuu wa gazeti la Tanzania Daima, Joseph Senga akiwa katika pozi na mke wake, Fridah Mockray mara baada ya kufunga ndoa katika Kanisa Katoliki Sinza jijini Dar es Salaam jana.
Mpiga Picha Mkuu wa gazeti la Tanzania Daima, Joseph Senga akipongezwa na mama yake mzazi
Pozi la harusi
Picha ya pamoja
Maharusi wakitoka Kanisani

 (Picha zote na Habari Mseto Blog)

Saturday, December 01, 2012

TAASISI YA MBUNGE CATHERINE MAGIGE YATOA MSAADA KWA WALEMAVU

 
Mbunge wa viti maalum bi Catherine Magige akisomama taarifa ya Foundation yake ilivyoanza kazi mbele ya mgeni rasmi mkuu wa wilaya na wananchi waliohudhuria uzinduzi wa Catherine Foundation kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya Arusha leo Asubuhi

 Mbunge wa viti maalum, Catherine Magige (katikati) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini ohn Mongela na wageni wengine meza kuu.
 Mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongela akiwa na mbunge wa viti maalum bi Catherine Magige wakiwa wanawakabidhi zawadi ya baiskeli walemavu watatu kwa niaaba ya walemavu 20 walipewa zawadi hizo
 Mbunge wa viti maalum, Catherine Magige wakiwa wanawakabidhi zawadi ya baiskeli walemavu watatu kwa niaaba ya walemavu 20
Mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongela akifanya mahojiano na vyombo vya habari mara baada ya kukamilika zoezi hilo. Picha na Mahmoud Ahma. 

PINDA ASHIRIKI MAZISHI YA MKE WA HAMAD RASHID

 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA na Kiongozi wa Upizani Bungeni, Freeman Mbowe katika mazishi ya Kisa Gwalugano Mohamed,Mke wa  Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam Novemba 29,2012.(Pich na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad katika mazishi ya Kisa Gwalugano hamad, Mke wa Mbunge wa Wawi yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam Novemba 29,2012. Kusshoto ni Waziri Mkuu Mstaafu, Salim Ahmed Salim na Wapili kulia ni Waziri  wa NchiOfisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
Waziri  Mkuu, Mizengo pinda akisalimiana na Mwenyekiti wa CUF,Ibrahim Lipumba katika mazishi ya Kisa Gwalugano Hamad , mke wa mbunge wa Wawi, Hamad Rashid yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam Novemba 29,2012.Kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu, Salim Ahmed Salim, Wanne kulia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif hamad Watatu kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu William Lukuvi na kulia ni Kiongozi wa UpinzaniBungeni, Freeman Mbowe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akiwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa  na serikali katika mazishi ya Kisa Gwalugano Mohamed, mke wa Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam Novemba  29,2012. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo,Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Waziri Mkuu Mstaafu, Salim Ahmed Salim, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad, Waziri wa Nchi Ofisi yaWaziri Mkuu, William Lukuvi na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
Waombolezaji wa wakiuzika mwili wa marehemu Kisa Gwalugano Mohamed yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam, Novemba 29,2012
 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda  na viongozi wa vyama vya siasa  na serikali wakimfariji, Mbunge wa Wawi, Hamd Rashid (wapili kulia) katika mazishi ya mkewe, Kisa Gwalugano Mohamed yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam, Novemba 29,2012. Kushoto ni mwenyekiti wa CUF, Profes Ibrahim Lipumba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU ASAFIRI KWA SGR KUELEKEA DODOMA

  Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Septemba 30, 2026 amesafiri kwa treni ya Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma. ...