Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
JETOUR Tanzania imezindua rasmi JETOUR Club pamoja na kutambulisha magari mapya ya JETOUR G700 na F700, ikiwa ni sehemu ya mpango wa “Africa Expedition 2025” unaolenga kuonesha uwezo wa magari hayo katika safari na mazingira mbalimbali barani Afrika.
Kwa mujibu wa JETOUR Tanzania, G700 ni SUV ya kifahari yenye mfumo wa mseto unaochajiwa kwa umeme (plug-in hybrid), ikiwa imeundwa kuunganisha nguvu, teknolojia ya kisasa, uwezo wa kusafiri umbali mrefu na utendaji unaoweza kukabiliana na mazingira yenye changamoto.
G700 inatumia injini ya petroli yenye turbo ya lita 2.0 pamoja na injini mbili za umeme na mfumo maalum wa upokezaji wa mseto, unaozalisha hadi kilowati 665, sawa na nguvu za farasi 904 na torque ya Nm 1,135.
JETOUR Tanzania imesema gari hilo lina uwezo wa kuongeza kasi kutoka kilomita sifuri hadi 100 kwa saa ndani ya takribani sekunde 4.6, huku likiwa na kasi ya juu ya kilomita 180 kwa saa, jambo linaloonyesha mchanganyiko wa utendaji wa juu na teknolojia ya mseto.
Kwa matumizi ya Afrika, G700 imejengwa kwa kuzingatia mazingira yenye changamoto, likiwa na muundo wa body-on-frame wenye uimara mkubwa, mfumo wa kuendesha magurudumu yote unaotumia injini mbili za umeme na nafasi ya chini kutoka ardhini ya milimita 230.
Aidha, kwa mujibu wa taarifa hiyo, G700 lina uwezo wa kupita kwenye maji yenye kina cha takribani milimita 900, huku likiwa na pembe ya kuingia kwenye kikwazo ya nyuzi 35 na pembe ya kutoka ya nyuzi 28, sifa zinazolenga kuongeza uwezo wake katika maeneo yenye barabara zisizo na lami na safari za nje ya miji.
Gari hilo pia lina mifumo mbalimbali ya kukabiliana na aina tofauti za ardhi, ikiwemo Snow, Mud, Sand na Rock, pamoja na Intelligent X Mode, Wading Mode, mfumo wa kusaidia kushuka mteremko, Off-Road Crawl na Tank Turn.
Kwa upande wa matumizi ya nishati, G700 ina betri ya lithium iron phosphate yenye uwezo wa 34.13 kWh, inayotoa umbali wa hadi kilomita 100 kwa kutumia umeme pekee kwa mujibu wa vipimo vya WLTC, na umbali wa pamoja unaofikia hadi kilomita 1,000.
JETOUR Tanzania imesema G700 pia ina mfumo wa kuchaji wa 800V wenye uwezo wa kuchaji kwa kasi ya hadi kW 170, huku ndani ikiwa na teknolojia ikiwemo skrini ya kugusa ya inchi 15.6, mfumo wa kudhibiti kwa sauti, Apple CarPlay na Android Auto, viti vya kiwango cha juu na panoramic sunroof.
Kwa upande mwingine, JETOUR F700 imeletwa katika kundi la pickup zenye utendaji wa juu, ikiwa na injini ya petroli ya turbo ya lita 2.0, injini mbili za umeme na mfumo wa upokezaji wa mseto wenye gia mbili unaozalisha hadi kilowati 665, nguvu za farasi 892 na torque ya Nm 1,135.
F700 ina mfumo wa kuendesha magurudumu yote muda wote, uwezo wa kupita kwenye maji yenye kina cha hadi milimita 900 na uwezo wa kuvuta mzigo wenye uzito wa hadi kilogramu 3,500, huku inverter yake ikiwa na uwezo wa kutoa hadi kW 20 za umeme kwa matumizi ya nje.
Kwa mujibu wa JETOUR Tanzania, G700 na F700 zimewekwa katika mkakati wa “Africa Expedition” unaolenga safari za umbali mrefu, utalii, shughuli za kifamilia, biashara na matumizi ya nje katika mazingira mbalimbali ya Afrika.









No comments:
Post a Comment