Tuesday, September 22, 2026

RAIS DKT. MWINYI AFIKA MBWENI KUTOA POLE KWA FAMILIA YA MAREHEMU MAMA FATMA KARUME

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akitoa pole kwa Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti Mstaafu wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Amani Abeid Karume, kufuatia kifo cha mama yake, Marehemu Mama Fatma Karume, nyumbani kwa familia hiyo Mbweni, Wilaya ya Magharibi “B”, Unguja, leo Septemba 22, 2026.





Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo tarehe 22 Septemba 2026 amefika nyumbani kwa familia ya Marehemu Mama Fatma Karume, Mbweni, Wilaya ya Magharibi “B”, Unguja, kutoa pole na rambirambi kufuatia msiba wa Mama Fatma Karume, mjane wa Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Rais wa Kwanza wa Zanzibar.

Katika ziara hiyo ya pole, Rais Dkt. Mwinyi amesaini kitabu cha maombolezo na kuifariji familia, akiwataka wanafamilia kuwa na subira, uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.

Rais Dkt. Mwinyi pia amewaomba ndugu, jamaa, marafiki na wananchi kuendelea kumuombea Marehemu Mama Fatma Karume, akimuomba Mwenyezi Mungu amrehemu, amsamehe na amjaalie makaazi mema Peponi.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mama Fatma Karume mahali pema Peponi na awajaalie wafiwa wote moyo wa subira na ustahamilivu. Amina.

No comments:

RAIS DKT. MWINYI AFIKA MBWENI KUTOA POLE KWA FAMILIA YA MAREHEMU MAMA FATMA KARUME

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi , akitoa pole kwa Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti...