ARUSHA, Septemba 28, 2026 — Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amewasili mkoani Arusha kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma (C-CEOs Forum 2026).
Kikao hicho kinachofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) kuanzia Septemba 28–30, 2026, kinawakutanisha viongozi wa taasisi na mashirika ya umma pamoja na wadau wengine kujadili namna ya kuongeza ufanisi, tija na thamani ya uwekezaji wa Serikali, sambamba na kuimarisha mchango wa mashirika hayo katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Zaidi ya washiriki 700, wakiwemo viongozi kutoka mashirika ya umma zaidi ya 300, wanatarajiwa kushiriki katika jukwaa hilo linaloratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.
NHC ni miongoni mwa taasisi zinazoshiriki kikao hiki, ikiwa ni sehemu ya mashirika ya umma yanayoshiriki mijadala kuhusu nafasi ya taasisi hizo katika kuchochea maendeleo, uwekezaji na utekelezaji wa Dira 2050.







No comments:
Post a Comment