Friday, September 04, 2026

PUMAGAS YAPAZA SAUTI NISHATI SAFI, YAANZA ZIARA YA MIKOA MITANO

Wafanyakazi wa Puma Energy Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja huku wakipeperusha bendera, ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa ziara ya PumaGas katika mikoa mitano nchini. Ziara hiyo imezinduliwa katika kituo cha Puma kilichopo Bunju, Dar es Salaam, tarehe 3 Septemba 2026, na itaendelea kwa wiki nane ikianzia Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na Dodoma, kabla ya kuhitimishwa rasmi jijini Mwanza. 



Katika kuunga mkono jitihada za kuhamasisha matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia, Puma Energy Tanzania imezindua ziara ya PumaGas itakayopita katika mikoa mitano nchini, ikiwa na lengo la kusogeza elimu na uelewa kuhusu matumizi ya nishati safi karibu zaidi na wananchi.

Uzinduzi wa ziara hiyo umefanyika katika kituo cha Puma kilichopo Bunju, Dar es Salaam, Septemba 3, 2026, ambapo wafanyakazi wa Puma Energy Tanzania waliashiria kuanza kwa safari hiyo kwa kupeperusha bendera.

Ziara hiyo ya wiki nane itaanzia Dar es Salaam, kisha kuelekea Pwani, Morogoro na Dodoma, kabla ya kuhitimishwa jijini Mwanza.

Hatua hiyo inaongeza nguvu katika juhudi za kuhamasisha jamii kuhamia katika nishati safi ya kupikia, ambayo ni muhimu katika kuboresha mazingira ya nyumbani na kuendeleza matumizi ya vyanzo vya nishati vinavyosaidia kupunguza athari kwa mazingira.

Kupitia ziara hiyo, PumaGas inalenga kuwa sehemu ya mabadiliko ya kuelekea matumizi endelevu ya nishati safi, huku ikisisitiza umuhimu wa wananchi kupata uelewa na fursa ya kutumia nishati bora ya kupikia.

Nishati safi, mazingira bora, maisha bora.

#PumaGas #NishatiSafi #CleanCooking #MazingiraBora #NishatiKwaMaendeleo #Tanzania

No comments:

PUMAGAS YAPAZA SAUTI NISHATI SAFI, YAANZA ZIARA YA MIKOA MITANO

Wafanyakazi wa Puma Energy Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja huku wakipeperusha bendera, ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa ziara ya Puma...