Thursday, February 12, 2026

DKT. MATARAGIO APOKELEWA RASMI WIZARA YA NISHATI




Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi Asilia, Dkt. James Mataragio ameripoti  na kupokelewa rasmi katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, mwanzoni mwa wiki hii.

Katika maboresho ya muundo wa Wizara ya Nishati yaliyofanywa na Mhe. Rais, Wizara imepata Makatibu Wakuu wawili. Mhandisi Felchesmi Mramba ameendelea na wadhifa wake kama Katibu Mkuu anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, huku Dkt. James Mataragio akiteuliwa kuwa Katibu Mkuu anayeshughulikia Mafuta na Gesi Asilia.

Mapokezi ya Dkt. Mataragio yameongozwa na Katibu Mkuu anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Felichesmi Mramba, yakihudhuriwa na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara, mapema leo tarehe 12 Februari, 2026.

No comments:

MMUYA: WANANCHI WANUFAIKE NA UWEKEZAJI WA NHC KUPITIA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Kaspar Mmuya, amekagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maghala unaotekelezwa na S...