Monday, September 22, 2025

KATIBU MKUU WA MADINI ATEMBELEA BANDA LA TUME YA MADINI KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA









Geita, Septemba 22, 2025

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba, ametembelea Banda la Tume ya Madini katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bombambili, Manispaa ya Geita.

Katika ziara hiyo, Mhandisi Samamba ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo pamoja na viongozi waandamizi wa Tume ya Madini wakiongozwa na Mwenyekiti wa Tume, Dkt. Janet Lekashingo, pamoja na Makamishna wa Tume, Mhandisi Theonestina Mwasha na Dkt. Theresia Numbi.

Ziara hiyo imelenga kukagua na kujionea ubunifu na teknolojia mbalimbali zinazotumika katika sekta ya madini, huku Tume ya Madini ikiendelea kutoa elimu kwa wananchi na wadau kuhusu fursa na wajibu wao katika maendeleo ya sekta hiyo.

No comments:

TARURA YATEKELEZA UJENZI WA KM 56 ZA BARABARA ZA LAMI ILALA KUPITIA DMDP II

‎Serikali kupitia Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imeanza kutekeleza ujenzi wa barabara zaidi ya Kilomita 56 kwa kiwango...