Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili kwa kishindo katika Uwanja wa Ndege wa Songwe tarehe 03 Septemba 2025, kuendelea na mikutano ya kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa chama hicho mkoani Songwe.
Mara baada ya kuwasili, Dkt. Samia alipokelewa kwa shangwe, nderemo na hamasa kubwa kutoka kwa mamia ya wananchi na makada wa CCM waliokuwa wamekusanyika kumlaki. Mapokezi hayo yameonyesha mshikamanano na matumaini makubwa kwa wananchi kuhusu safari ya kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Ziara ya Dkt. Samia mkoani Songwe inalenga kuzungumza moja kwa moja na wananchi, kueleza dira na mikakati ya maendeleo ya awamu ijayo, huku akisisitiza dhamira ya kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika uongozi wake.
#Samia2025 #Songwe #CCM #UchaguziMkuu2025 #KaziInaendelea
No comments:
Post a Comment