Sunday, September 21, 2025

Makamu wa Rais Dkt. Mpango Awasili Marekani kwa Kikao cha UNGA 80











Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, leo tarehe 21 Septemba 2025 amewasili jijini New York, Marekani.

Dkt. Mpango yupo nchini humo kwa ajili ya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Kikao cha 80 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA 80).

Tanzania kupitia ushiriki huu inaendelea kushirikiana na mataifa mbalimbali duniani katika kujadili masuala muhimu ya maendeleo, diplomasia, uchumi na ustawi wa dunia.


Tanzania mbele kwenye majukwaa ya kimataifa!



No comments:

RAIS DKT. SAMIA AKUTANA NA UJUMBE WA JUKWAA LA MABUNGE LA NCHI ZA MAZIWA MAKUU (FP-ICGLR) IKULU NDOGO TUNGUU, ZANZIBAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Kiongozi wa Jukwaa la Mabunge la...