Monday, September 29, 2025

Mwili wa Hayati Askofu Mkuu Rugambwa wapokelewa Bukoba







Mwili wa Hayati Askofu Mkuu Novatus Rugambwa, aliyefariki hivi karibuni, uliwasili leo katika Kanisa Kuu la Bikira Maria wa Huruma, Jimbo Katoliki Bukoba, na kupokelewa kwa heshima kubwa na waumini pamoja na viongozi wa Kanisa Katoliki.

Waumini kwa mamia walijitokeza kuupokea mwili huo, huku ibada maalum ya kumuombea ikiongozwa na viongozi wa Kanisa, ikihudhuriwa pia na viongozi wa Serikali, wawakilishi wa madhehebu mbalimbali pamoja na wananchi.

Katika hotuba zao, viongozi wa dini walimsifu Hayati Askofu Mkuu Rugambwa kwa uongozi wake thabiti, hekima, na moyo wa utumishi uliogusa maisha ya wengi, si tu ndani ya Kanisa, bali pia katika jamii kwa ujumla.

Waumini waliendelea kumwombea marehemu apumzike katika amani ya Bwana, huku taratibu za mazishi zikitarajiwa kuendelea katika siku chache zijazo.

No comments:

NAIBU WAZIRI WA FEDHA AMWAKILISHA WAZIRI WA FEDHA KATIKA KONGAMANO LA 16 LA MWAKA LA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI – ARUSHA

Naibu Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Mhandisi Mshamu Ali Munde, amemwakilisha Waziri wa Fedha katika ufunguzi wa Kongamano la 16 la Mwaka la Wa...