Tuesday, April 08, 2025

WAZIRI NDEJEMBI ASITISHA UUZWAJI ARDHI ENEO LA MAHOMANYIKA









Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi amesitisha mara moja uuzaji wowote wa kipande cha ardhi eneo la Mahomanyika mpaka ufumbuzi wa mgogoro katika eneo hili utakapopatikana.

Waziri Ndejembi amesema hayo Aprili 8, 2025 jijini Dodoma katika mkutano wa hadhara na wananchi wa eneo la Mahomanyika ili kutoendeleza migogoro ya ardhi katika eneo hilo.

“Njia ya kupata tiba ni kuanzia leo April 08, 2025, nasitisha uuzaji wowote, na kusiwe na mwenyekiti yeyote wa mtaa ambaye atajitokeza kuuza eneo. Kwanza hakuna Mwenyekiti wa Mtaa mwenye ardhi, ardhi ni ya wanananchi” amesema Waziri Ndejembi.

Waziri Ndejembi ameongeza kuwa ardhi yote ni ya mtaa hivyo ni lazima mkutano ufanyike ili wananchi wakubaliane linakatwa eneo gani na neo hilo linauzwa kulingana na taratibu za kuuza ardhi ya Kijiji.

Aidha, Waziri Ndejembi amesema ataunda timu ya kuchunguza mgogoro huo ndani ya siku 14 ambapo jiji la Dodoma ambalo linalalamikiwa na wananchi halitahusika na badala yake timu hiyo itaundwa na wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakiongozwa na Kamishna wa Ardhi Bw. Nathaniel Nhonge pamoja vyombo vya ulinzi na usalama ambapo watapitia nyaraka zote ili kujua kila kipande cha ardhi na mmiliki wake.

Waziri Ndejembi amesema katika zoezi hilo hatarajii kuwaona mamluki, ikigundulika kuna yeyote, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake na hana nia ya kumaliza mgogoro huo.

“Nikiangalia hawa wana Mahomanyika, hawana ubaya na kupima maeneo yao, wanataka maendeleo na wao waishi katika maeneo yaliyopangwa, nikiwasililiza vizuri wana Mahomanyika, wanataka ushirikishwaji katika upangaji ule na wajue wao kama wenyeji wasisukumwe nje ya maeneo yao na wao wawepo kuendeleza maendeleo ya eneo lao walipozaliwa” amesema Waziri Ndejembi

No comments:

HELIUM ONE YAKAMILISHA MALIPO YA FIDIA KWA WANANCHI WA ITUMBULA

  ● Yalipa fidia ya shilingi zaidi ya milioni 100 kwa wananchi ● Wananchi wafurahishwa na maendeleo ya mradi ● Mradi kutekelezwa kwa kipindi...