Sunday, April 06, 2025

WAZIRI MKUU AWATAKA MABALOZI KUISHI FALSAFA ZA RAIS DKT. SAMIA




WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka mabalozi kuiishi falsafa ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuimarisha mahusiano na kukuza diplomasia ya kiuchumi kati ya Tanzania na mataifa mbalimbali duniani.

Mheshimiwa Majaliwa amesema kufanya hivyo kutaiwezesha Tanzania kuvutia wawekezaji katika sekta mbalimbali zikiwemo za viwanda, kilimo, biashara pamoja na kupata masoko ya bidhaa zinazozalishwa nchini.

Ameyasema hayo leo (Jumapili, Aprili 6, 2025) alipokutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Balozi Hamad Khamis Hamad Balozi wa Tanzania nchini Msumbuji na Mheshimiwa Balozi Mobhare Matinyi, Balozi wa Tanzania nchini Sweden.

Mheshimiwa Majaliwa amesema Serikali ina mategemeo makubwa na mabalozi hao, hivyo wanapaswa kwenda kuendeleza mahusiano mazuri ya muda mrefu yaliyopo baina ya Tanzania na mataifa hayo.

Waziri Mkuu amesema pamoja na mambo mengine mabalozi hao wanatakiwa wahakikishe wanasimamia vizuri matumizi ya fedha katika ofisi zao pamoja na kuanzisha au kuendeleza madarasa ya kufundisha lugha ya kiswahili.

No comments:

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Aungana na Watanzania Kusafiri kwa Treni ya Umeme ya Kiwango cha Kimataifa (SGR)

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), ameandika historia mpya mnamo Agosti 18, 2025, b...