Thursday, April 10, 2025

RAIS SAMIA KUZINDUA BENKI YA USHIRIKA


Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Aprili 10,2025 jijini Dodoma kuelekea uzinduzi wa Benki ya Taifa ya Ushirika utakaofanyika Aprili 28,2025.

Na. Alex Sonna-DODOMA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan,anatarajia kuzindua rasmi Benki ya Ushirika mnamo Aprili 28,2025 jijini Dodoma.

Hayo yamesemwa leo Aprili 10,2025 jijini Dodoma na Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe,wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuelekea katika uzinduzi wa Benki hiyo.

Waziri Bashe amebainisha kuwa uzinduzi wa Benki hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya hatua za kuimarisha, kuendeleza Ushirika na kuinua sekta ya Kilimo.

“Benki hiyo inaanza kazi ikiwa na Mtaji wa Shillingi Bilioni 55, wakati Wanaushirika wakimiliki wa Hisa kwa asilimia 51na Wadau wengine, Sekta Binafsi asilimia 49.”amesema Mhe.Bashe

Aidha amesema kuwa Benki hiyo ya Ushirika tayari inafanya kazi katika Matawi ya Dodoma, Kilimanjaro, Mtwara na Tabora.

Katika hatua nyingine Waziri Bashe  amezindua Tovuti ya Usajili kwaajili ya washiriki wa uzinduzi huo yenye anuwani www.coopbanklaunch.co.tz

Uzinduzi wa Benki hiyo utatanguliwa na Kongamano la Wanaushirika na wadau Aprili 27, 2025

No comments:

HELIUM ONE YAKAMILISHA MALIPO YA FIDIA KWA WANANCHI WA ITUMBULA

  ● Yalipa fidia ya shilingi zaidi ya milioni 100 kwa wananchi ● Wananchi wafurahishwa na maendeleo ya mradi ● Mradi kutekelezwa kwa kipindi...