Thursday, April 10, 2025

USSI-WAFUGAJI WACHANGAMKIE FURSA YA SOKO MACHINJIO YA KISASA VIGWAZA




Mwamvua Mwinyi, Chalinze, April 10,2025

Wafugaji wa mifugo mbalimbali ,wametakiwa kuchangamkia fursa ya soko la ndani na nje ya nchi kupitia machinjio ya kisasa ya Union Meat Abattoirs Ltd, yaliyopo katika kijiji cha Kwazoka, Vigwaza, Halmashauri ya Chalinze, mkoani Pwani.

Machinjio hayo, ambayo yamegharimu zaidi ya sh.bilioni 26, huzalisha bidhaa za nyama zinazouzwa ndani ya Tanzania na kusafirishwa hadi nchi za Qatar, Oman na Bahrain.

Akizungumza Aprili 10, 2025, wakati wa ziara ya Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Chalinze, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2025, Ismail Ali Ussi, alieleza kuwa Tanzania inaendelea kuwa mdau mkubwa katika uzalishaji na usambazaji wa bidhaa za nyama, ndani na nje ya nchi.


“Kipindi cha miaka ya nyuma wafugaji walikosa masoko, lakini kwa sasa kuna fursa kubwa kupitia uwekezaji wa ndani, Ni wakati wao kutumia fursa hii kunufaika kiuchumi,” alisema Ussi.

Vilevile alieleza ,mafanikio hayo yanatokana na juhudi na mapinduzi ya maendeleo yanayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana na viongozi wa halmashauri, wilaya na wabunge katika maeneo husika.

Ussi pia alipongeza kampuni ya Union Meat Group kwa uwekezaji wake mkubwa na hatua ya kusogeza huduma na masoko karibu na wafugaji.

Awali Mkurugenzi wa machinjio ya kisasa Vigwaza, Mariam Mnghwani alifafanua, machinjio hiyo ina uwezo wa kuchinja ng’ombe 300 kwa mstari mmoja kwa siku na kondoo 3,000.
Pia ina uwezo wa kuhifadhi tani 150 kwa mara moja na mradi huo unazalisha tani tatu kila siku na kuzalisha mifupa, ngozi kuuzia Wananchi wenye uhitaji. 
Mariam alisema kuwa, ujenzi wa mradi ulianza septemba 2022 , ambapo agost 2024 ulikamilika na kufika novemba 2024 machinjio ilianza kazi. 
Akipokea mwenge wa Uhuru kutokea Kibaha, mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Shaibu Ndemanga alieleza, miradi saba imetembelewa halmashauri ya Chalinze yenye thamani ya zaidi ya bilioni 28.9.
Katika miradi mingine iliyopitiwa na mwenge wa Uhuru ni ujenzi wa vyumba vya biashara kituo cha mabasi cha Chalinze mradi unaotekelezwa na halmashauri ya Chalinze wenye vyumba 50 vya biashara ,stendi ya mabasi Bwilingu, utakaogharimu milioni 216.5.
Mradi wa ujenzi wa shule ya Amali Msoga na mradi wa uwekaji taa 50 za barabarani kijiji cha Ruvu kata ya Vigwaza uliogharimu milioni 185.

No comments:

TANZANIA AND BURKINA FASO IN TALKS TO ESTABLISH CARDIAC FACILITY MODELED AFTER JAKAYA KIKWETE CARDIAC INSTITUTE

  On April 17, 2025, in Ouagadougou, the Executive Director of Muhimbili National Hospital, Prof. Mohamed Janabi @ProfJanabi, along with the...