Friday, April 04, 2025

MAKAMU WA RAIS MHE. DKT. PHILIP MPANGO AONGOZA KIKAO CHA 15 CHA KAMATI YA PAMOJA YA MASUALA YA MUUNGANO




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango, ameongoza Kikao cha 15 cha Kamati ya Pamoja kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) cha kushughulikia masuala ya Muungano. Kikao hiki kimefanyika leo, tarehe 04 Aprili 2025, katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu, Jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo umejikita katika kujadili na kutafuta suluhisho kwa changamoto mbalimbali zinazohusu Muungano, huku ukilenga kuimarisha mshikamano, ushirikiano, na maendeleo kati ya pande mbili za Muungano. Viongozi wa pande zote mbili wameonyesha dhamira ya dhati ya kuhakikisha masuala yanayohusu Muungano yanashughulikiwa kwa ufanisi na kwa manufaa ya Watanzania wote.

No comments:

WAZIRI NA NAIBU WAZIRI WA ARDHI WASHIRIKI KIKAO CHA KWANZA CHA MKUTANO WA 19 WA BUNGE LA 12 KWA AJILI YA KUJADILI BAJETI YA SERIKALI 2025/2026

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi (MB), leo tarehe 8 Aprili 2025, ameshiriki kikao cha kwanza cha Mku...