Sunday, April 13, 2025

*TANAPA YASHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 103 YA KUZALIWA KWA MWL. NYERERE – DODOMA





Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), likiongozwa na Kamishna wa Uhifadhi Musa Nassoro Kuji, limeshiriki hafla ya Maadhimisho ya Kumbukizi ya Miaka 103 ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere, leo Aprili 13, 2025, yanayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Dkt. Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango, pamoja na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakiongozwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Danstan Kitandula (Mb).

Sherehe hizo zimeandaliwa na Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwl. J.K. Nyerere, ambapo TANAPA ni Mdhamini Mkuu wa Maadhimisho hayo. Kaulimbiu ya Maadhimisho haya ni: “Chagua Viongozi Bora kwa Ustawi wa Jamii na Maendeleo Endelevu ya Taifa.”

Katika kuenzi misingi ya uongozi wa Mwalimu Nyerere na Azimio la Arusha ambalo lililenga kujenga jamii yenye misingi ya uadilifu, usawa, uwajibikaji na uzalendo limekuwa likienziwa hivyo kupitia maadhimisho hayo, Watanzania wamehimizwa kuendeleza maono ya Baba wa Taifa kwa kusimamia rasilimali za nchi kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho, sambamba na kuchagua viongozi bora watakaoendeleza misingi hiyo kwa maendeleo endelevu ya Taifa.

Aidha, TANAPA imetumia jukwaa hilo kuhamasisha Watanzania kupigia kura Hifadhi za Taifa kumi (10) zilizoingia katika vipengele vinane (8) katika kuwania Tuzo kubwa za Utalii Duniani, maarufu kama World Travel Awards, ili kuendelea kuitambulisha Tanzania kimataifa jambo linalotarajiwa kuchochea ongezeko la watalii na mapato yatokanayo na shughuli za utalii.

No comments:

HELIUM ONE YAKAMILISHA MALIPO YA FIDIA KWA WANANCHI WA ITUMBULA

  ● Yalipa fidia ya shilingi zaidi ya milioni 100 kwa wananchi ● Wananchi wafurahishwa na maendeleo ya mradi ● Mradi kutekelezwa kwa kipindi...