Wednesday, April 16, 2025

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIUNDOMBINU YA BARABARA YA DAR ES SALAAM – LINDI






Waziri Mkuu wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa, amefanya ziara ya kukagua miundombinu ya barabara kuu ya Dar es Salaam – Lindi, iliyoharibiwa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

Waziri Mkuu ameambatana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stegomena Tax, na Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ambapo walijionea hali halisi ya barabara hiyo na hatua zinazochukuliwa ili kurekebisha na kuimarisha miundombinu hiyo muhimu.

Ziara hii ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita kuhakikisha miundombinu ya barabara inaboreshwa na kudumishwa ili kuwezesha usafirishaji salama na wa haraka kwa wananchi na bidhaa muhimu.

#Tanzania #Miundombinu #WaziriMkuu #Somanga #Ujenzi #SerikaliYaAwamuYaSita #Barabara

No comments:

BILIONI 51 KUTUMIKA UJENZI WA BARABARA, MASOKO NA STENDI JIJINI ARUSHA

Mradi wa Uendelezaji wa Miji na Majiji Tanzania (TACTIC) unatekeleza miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 51 katika Jiji la Arusha ikiwa...