Mrembo atakaeiwakilisha Tanzania
katika mashindano ya mwaka huu ya urembo ya Miss East Africa atatangazwa
rasmi tarehe 14/10/2012 katika hotel ya Serena Jijini Dar es salaam.
Jumla ya warembo 148 wameomba
kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss East Africa mwaka huu
lakini ni Mrembo mmoja tu atakaechaguliwa kuiwakilisha Nchi katika
mashindano hayo makubwa ya urembo katika ukanda huu wa Africa na
yanayosubiliwa kwa hamu na wapenzi wa fani hiyo ndani na Nje ya Africa
Mashariki
Aidha maandalizi ya mashindano
hayo yanaendelea vizuri ambapo yatafanyika tarehe 07 December, 2012
katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam
Wakati huohuo Nchi ya Burundi
imebadili mwakilishi wake ambapo sasa itawakilishwa na mrembo Ariella
Kaneza (23), Mwanafunzi wa mwaka wa pili wa chuo kikuu cha Universte De
Lumiere akichukua Degree ya marketing.
Taarifa kutoka Burundi
iliyosainiwa na Mratibu wa Mashindano ya Miss East Africa Nchini humo,
Serge Nkurunziza, zimeeleza kwamba Burundi imeamua kubadili mwakilishi
wake ili kuhakikisha kwamba Nchi hiyo inashinda Taji hilo kwa mara ya
pili tangu mashindano hayo yalipoanzishwa mwaka 1996 baada ya kugundua
kwamba mwakilishi wake wa awali anapungukiwa baadhi ya sifa chache za
kuweza kunyakua taji hilo. (Burundi imewahi kushinda Taji hilo mara moja
mwaka 2008 kupitia kwa mrembo wake Miss Claudia Niyonzima)
Mashindano ya Miss East Africa
mwaka huu yanatarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake na yatashirikisha
warembo kutoka Nchi 16 za ukanda wa Afrika Mashariki.
Nchi
zilizothibitisha kushiriki mashindano hayo ni wenyeji Tanzania, Kenya,
Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi zingine zilizoalikwa kushiriki ni pamoja
na Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, Southern Sudan, Malawi, pamoja
na visiwa vya Seychelles, Madagascar, Reunion, Comoros, na Mauritius.
Mashindano ya Miss East Africa
yanalenga kukuza ushirikiano na kutangaza utamaduni wa Afrika Mashariki,
pamoja na kutangaza utalii wa Tanzania kama Nchi wenyeji wa mashindano
hayo makubwa katika ukanda huu wa Afrika
Mashindano ya Miss East Africa yanamilikiwa na kuandaliwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam,.
No comments:
Post a Comment