.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeshinda uchaguzi mdogo wa jimbo la Bububu, Zanzibar.
Akitangaza matokeo Misimamizi wa Uchaguzi huo
Suluhu Ali Rashid amesema kuwa Hussein Ibrahim Makungu wa CCM ameshinda kwa
kupata kura 3371 sawa sawa na asilimia 50.7ambapo Issa Khamis Issa wa CUF
amepata kura 3204 sawa sawa na asilimia 48.2
Aidha Suluhu amesema kuwa Mgombea wa Chama cha
ADC Zuhura Bakari Mohamed amepata kura 45 sawa sawa na asilimia 0.7 wakati
Abubakar Hamad Said wa Chama cha AFP amepata kura 8 sawa sawa na asilimia 0.1,
Mtumweni Jabir Seif wa Jahazi Asilia amepata kura 7 sawa sawa na asilimia
0.1,Haroun Abdulla Said wa NCCR amepata kura 3 sawa sawa na asilimia 0.0,
Suleiman M.Abdulla wa NRA amepata kura 1 sawa sawa na asilimia 0.0 Seif Salim
Seif amepata kura tatu sawa sawa na asilimia 0.0 na Juma Metu Domo wa Chama cha
SAU amepata kura 4 sawa sawa na asilimia 0.1.
Jumla ya kura 6720 zilipigwa sawa sawa na
asilimia 68.6.Kura 74 ziliharibika sawa sawa na asilimia 1.1Kura halali
ziliozopigwa zilikuwa 6646 sawa sawa na asilimia 98.9na waliojiandikisha
walikuwa 9799.
No comments:
Post a Comment