Balozi
wa tamasha la Tanzania Live Music Festival Jackline Wolper akizungumza
na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Leaders leo wakati wandaaji wa
tamasha hilo walipozungunzia kukamilika kwa maadalizi katika picha
wanaofuatia ni Mzee King Kikii, Tarsis Masela wa Akudo Impact na
Jamwaka kutoka Sikinde
……………………………………….
Tanzania Live Music Festival
imewadia! ambapo kuanzia kesho tarehe 28/29 mashabiki wote wa muziki wa
dansi jijini Dar es saalam wanakaribishwa kuburudika na muziki wa wa
dansi bila kikomo,katika viwanja vya Leaders jijini ikijumuisha bendi
zaidi ya kumi ambazo zitakuwa zikiimba live.
Bendi zitakazo tumbuiza ni Sikinde, Msondo, B Band Mashujaa Band, Akudo, FM Academia, Wazee Sugu na wengine kibao!
Lakini pia kutakuwa na bendi
zitakazosindikiza onesho hilo kama vile Khadija Kopa malikia wa Mipasho
na Mashauzi Classic chini ya Isha Mashauzi.
Lengo kubwa la Tamasha hili ni kusaidia Chama cha Dansi Tanzania CHAMUDATA ili kuboresha na kuendeleza chama hicho.
waandaajiwa tamasha hilo wametoa
shukurani kwa Kampuni zote ambazo zimekuwa zikiunga mkono maadalizi
yote ili kufanikisha Tamasha hili.
Kampuni hizo ni
TIMES FM, GLOBAL PUBLISHERS, MAJIRA, WHINDHOEK, REAL STAR, FLY 540, FACE TO FACE BAR and RESTAURANT, PUSH MOBILE
Wapenzi wote wa muziki wa dansi
mnakaribishwa kujiunga pamoja na kupata burudani. Kiingilio ni 20,000
kwa VIP na 5000 kwa tiketi za kawaida. Wote mnakaribishwa.
No comments:
Post a Comment