Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akijiridhisha kwa kupima kiwango cha lami
inayowekwa upya katika barabara ya Kilwa na Kampuni ya Kajima ya Japan
leo jijini Dar es salaam. Wengine wanaoshuhudia kutoka kulia ni mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki, Balozi wa Japani nchini
Tanzania Masaki Okada na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Kajima.
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akikagua ujenzi wa daraja la Kigamboni
akiwa ameambatana na viongozi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Mecki Sadiki (wa pili kutoka kulia)
Mbunge wa Kigamboni Dkt.Faustine Ndugalile (wa tatu kutoka kulia) leo
jijini Dar es salaam. Daraja la Kigamboni linajengwa na kampuni ya
China Railways Engineering kwa gharama ya shilingi bilioni 214 na
linatarajia kukamilika kabla ya mwaka 2015
Mmoja
wa wafanyakazi wa daraja hilo ambaye jina lake halikupatikana mara
moja akiendelea na zoezi la kupiga picha huku akiwa amesimama kwenye
mtando unaopitisha umeme mwingi bila kuchukua tahadhali wakati waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli alipokua akikagua maendeleo ya ujenzi wa
daraja hilo leo.
Picha na Aron Msigwa -MAELEZO
No comments:
Post a Comment