Tuesday, September 04, 2012

Jamani jamani hivi nchi yetu tunaipeleka wapi?

 Askari (kushoto), anaonekana kumwelekezea mtutu tumboni.







Jamani hebu angalieni mauaji haya ya kutisha ya Mwandishi wa Habari Daud Mwangosi, hakika ni tukio lisilokubalika na la kusikitisha duniani na hata mahala pengine kokote kule. Hivi tujiulize chanzo cha mauaji haya, kwanini Polisi watumie nguvu na kwanini pia wananchi wawalazimishe polisi watumie nguvu. Na je hivi wanaosababisha maafa haya yote kwanini wasichukuliwe hatua kali.

Inawezekana kabisa viongozi watawala, mihimili ya dola nayo imekuwa wapole saana natamani Watanzania wangeona kazi ya (ukatili) wa POLISI wa KENYA au SOUTH AFRICA . wangewaheshimu sana Polisi wetu na kusingetokea haya yanayotokea katika hizo nchi polisi hana muda hata kidogo wa kubishana na raia. 

Tanzania sasa hivi tunajenga utamaduni wa ajabu wa kila mmoja kuwa kambale, zinapozungumza mamlaka halali za nchi wananchi wanapinga na wakati mwingine wanapozungumza raia halali wa nchi na pengine madai halali, mamlaka zinapinga sijui utamaduni huu utatufikisha wapi???? Matokeo yake ni kwamba nchi inakuwa kama soko kila mtu anasema lake ni hatari mnooo.

No comments:

LIPUMBA AWAPA NENO WAJUMBE MKUTANO MKUU CUF

  Na Mwandishi Wetu  MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amewaelekeza wajumbe wa Baraza Kuu la chama hic...