Monday, May 05, 2014

KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS 2014 MLIMANI CITY JIJINI DAR

Mshindi wa tuzo saba za KTMA Diamond akikabidhiwa tuzo na staa wa filamu Bongo, Vincent Kigosi 'Ray'.
...Akikabidhiwa tuzo na mchumba wake Wema Sepetu.
...Akipokea tuzo kutoka kwa George Kavishe.
...Akipozi na mpenzi wake Wema Sepetu.
...Akiwa na Nay wa Mitego baada ya tuzo yao ya Wimbo Bora wa Kushirikisha/Kushirikiana ambao ni Muziki Gani.
Diamond akipokea tuzo kutoka kwa prodyuza Tuddy Thomas.
Shabiki wa Diamond akimpongeza kwa kutwaa tuzo nyingi.
...Akipokea tuzo nyingine kutoka kwa 'shemeji yake' Martin Kadinda.
...Akikumbatiana na mpenzi wake Wema kabla ya kupewa tuzo.
...Akiwashukuru mashabiki.
Msanii Ray C akikabidhi tuzo kwa Nikki wa Pili ambaye ni memba wa Weusi.
Weusi wakiwa na tuzo yao ya Kikundi Bora cha Mwaka, Kizazi Kipya.
Msanii Bora wa Hip hop na Mtunzi Bora wa Mwaka Hip hop, Farid Kibanda 'Fid Q' baada ya kutwaa tuzo zake mbili.
Mwimbaji Bora wa Kike Taarab na Mtumbuizaji Bora wa Kike wa Muziki, Isha Ramadhan 'Mashauzi' akiwa na mojawapo ya tuzo zake.
Msanii Young Killer akipokea tuzo yake ya Msanii Bora Chipukizi Anayeibukia kutoka kwa msanii JB.
...Killer akiwashukuru mashabiki.
Man Water kutoka Combnation Sound akiwa na tuzo yake ya Mtayarishaji Bora wa Nyimbo wa Mwaka, Kizazi Kipya.
Mwanadada Vanessa Mdee akiwa na tuzo yake ya Wimbo Bora wa RnB aliyokabidhiwa na Elizabeth Michael 'Lulu'.
Mwimbaji Bora wa Kike Bendi, Luiza Mbutu (katikati) akiwa na tuzo yake aliyokabidhiwa na wasanii kutoka Kenya, Amani na Kelvin Wyre.
Mtunzi Bora wa Mwaka Bendi, Christian Bella akipokea tuzo yake kutoka kwa Issa Michuzi.
Mashujaa wakipozi na mojawapo ya tuzo zao.

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shy Rose Bhanji Asherehekea Siku Yake Ya Kuzaliwa, Waheshimiwa Wabunge Halima Mdee na Easte Bulaya Waudhuria

  Shy-Rose akila pozi na keki aliyozawadiwa na mmoja wa marafiki zake.
  Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shy Rose Bhanji katikati akipokea keki kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki zake wakati wa tafrija maalum ya kumpongeza baada ya kutimiza miaka yake kadhaa katika ulimwengu huu Mei 3, 2014. Tafrija hiyo ilifanyika nyumbani kwake Bweni Dar es Salaam.
 Birthday Girl! Shy-Rose akikata akijiandaa kukata keki...
  Marafiki zake wa karibu ambao pia ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ester Bulaya (kushoto) na Halima Mdee wakimlisha keki kwa pamoja Shy-Rose.
 Shy-Rose nae aliwalisha marafiki zake ambao ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ester Bulaya (kushoto) na Halima Mdee

Mbunge wa Bunge la Afrika mashariki Akilishwa Keki na ndugu jamaa na marafiki
Shy-Rose Bhanji a.ak.a Mbunge wa Afrika Mashariki akila pozi na marafiki zake Halima Mdee a.k.a Mbunge wa Mujini na Ester Bulaya a.k.a Mbunge wa Kijijini .....ndivyo utani wao ulivyokuwa wakitaniana.Photos by: MD Digital Company +255 755 373999

Vigogo wa CCM Waung'uruma Kwenye mkutano wa CCM kwenye viwanja vya Kibanda Maiti, Unguja Zanzibar Nakusema Serikali Mbili Zatosha,Tatu Za Nini?

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Zanzibar na kuwaambia CCM itasimamia haki za Wazanzibar na kuhakikisha Muungano unadumu na Mapinduzi ya Zanzibar yanaenziwa .
 Wananchi wakionyesha ishara ya Serikali mbili kwenye mkutano wa CCM kwenye viwanja vya Kibanda Maiti, Unguja Zanzibar.
 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na watoto Ummy Mwalimu akionyesha ishara ya serikali mbili wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya kibanda maiti na kuwataka wanawake wote wa Zanzibar kuungana katika kusimamia Muungano wa Tanzania.
 Mbili zatosha.
 Kila mtu alionyesha mapenzi yake kwa CCM.
 Wakazi wa Zanzibar hawakujali mvua iliyokuwa inanyesha kwenye mkutano wa CCM Kibanda Maiti Zanzibar
 Mama Fatma Karume akihutubia wakazi wa Unguja na kuwaambia kuwa waasisi wetu waliweka uzio wa kutulinda na kudumisha umoja na undugu wetu na kusema uzio huo ni Muungano wetu.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mbunge wa Bunda Stephen Wassira akihutubia wananchi wa Zanzibar ambapo alisema UKAWA wanatakiwa kuelewa misingi ya Muungano kwanza kisha waje na hoja .
Mbunge wa Songea Mjini Dk Emmanuel Nchimbi akihutubia wakazi wa Unguja kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kibanda Maiti na kuwataka wananchi hao kuwa makini na viongozi wanaogeuza maneno huku akitolea mfano kutoka kwenye kitabu cha Maalim Seif.
Katibu wa NEC  Oganizeshen Dk. Mohamed Seif Khatibu akihutubia wakazi wa Unguja kwenye mkutano wa hadhara Kibanda maiti .
Sehemu ya Umati uliohudhuria mkutano wa hadhara ambao ulihutubiwa na Viongozi mbali mbali wa CCM wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.Picha na Adam Mzee
--
  • Wananchi wa Zanzibar wasema serikali mbili zatosha
  • Wachukizwa na wanasiasa wanafiki wanaopindisha pindisha maneno
  • Vijana wa CCM kutovumilia wanasiasa wanaokashifu waasisi wa Taifa letu
  • Wasema wamechoshwa na matendo ya Viongozi wa Vyama vya Upinzani wataka muswada wa kuujadili Serikali wa Umoja wa kitaifa wataka ufutwe kwani hauna faida kwa maendeleo yao .

SHEIKH ILUNGA KAPUNGU AFARIKI DUNIA

Sheikh Ilunga Hassan Kapungu enzi za uhai wake.
SHEIKH Ilunga Hassan Kapungu ameafariki dunia usiku wa kuamkia leo kwa ugonjwa wa kisukari jijini Dar es Salaam. Mazishi yake yatafanyika leo Jumatatu saa 10 jioni. Mwili wa marehemu utasaliwa katika msikiti wa Kichangani, Magomeni-Mapipa jijini Dar.
Taarifa hii imetolewa na:
Sheikh Mohammed Kassim,
IPC Ubungo
Dar es Salaam

Friday, May 02, 2014

RAIS KIKWETE ONGOZA MAADHIMISHO YA MEI MOSI JIJINI DAR ES SALAAM

MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI MKOANI RUKWA KATIKA UWANJA WA NELSON MANDELA MJINI SUMBAWANGA

Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mkoani Rukwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Methew Sedoyyeka (katikati) akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiimba kwa pamoja wimbo maarufu wa Wafanyakazi wa “Solidarity Forever”  na wafanyakazi walioshiriki maadhimisho hayo katika uwanja wa Nelson Mandela Mjini Sumbawanga.
Baadhi ya viongozi wa vyama vya wafanyakazi Mkoa wa Rukwa wakiwaongoza wafanyakazi kuimba wimbo wa uishirikiano baina yao “Solidarity Forever” katika kuadhimisha Siku ya wafanyakazi duniani ambayo Kimkoa imefanyika mjini Sumbawanga katika uwanja wa Nelson Mandela.
Maandamano katika kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani Mkoani Rukwa katika uwanja wa Nelson Mandela Mjini Sumbawanga.
Wafanyakazi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo.
Chuo cha Ufundi Stadi VETA Katandala.
Idara ya Maji Sumbawanga (RUKWA) wakifanya vitu vyao.
NMB Sumbawanga.
SIDO Rukwa.
Chuo Kikuu Huria tawi la Rukwa.
Onyesho lililohusisha watoto wachanga mapacha katika kuonyesha utoaji huduma kwa mama wajawazito na watoto wachanga katika Hospitali Kuu ya Rufaa ya Mkoa wa Rukwa.
Onyesho la uharibifu wa mazingira kwa uchomaji misitu na ukataji miti ambalo hupelekea nchi kuwa jangwa na kuua vyanzo vya maji. Onyesho hili liliandaliwa na Idara ya Maji Rukwa.
Kikundi cha Ngoma za asili cha Kanondo kikiburudisha katika maadhimisho hayo.
Kikundi cha Waalimu kikiimba wimbo wa kutetea haki za wafanyakazi.
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

NMB YATOA SOMO LA KUJENGA MITAJI, YAHIMIZA AKIBA YENYE MALENGO

  DODOMA. Benki ya NMB imewataka Watanzania kujenga utamaduni wa kuweka akiba kwa malengo na kufanya maamuzi sahihi ya uwekezaji ili kuimari...