Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 15 Aprili 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth), ambaye pia ni Rais wa zamani wa Jamhuri ya Malawi, Mhe. Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo yao yamejikita katika kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi, pamoja na kuendeleza ajenda za pamoja ndani ya Jumuiya ya Madola.
Mkutano huo unaakisi dhamira ya Tanzania kuendelea kujenga mahusiano imara ya kidiplomasia na washirika wa kimataifa, sambamba na kuimarisha nafasi yake katika jukwaa la kimataifa.
#SamiaSuluhuHassan #Tanzania #Commonwealth #Diplomasia #Maendeleo






No comments:
Post a Comment