Mheshimiwa Ryzhenkov amewasili kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, ambapo alipokewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe, pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Belarus nchini Mhe.Dzmitry Krasouski.
Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Ryzhenkov anatarajiwa kufanya mazungumzo ya pande mbili na mwenyeji wake, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Aprili 28, 2026, jijini Dar es Salaam. Aidha, atakutana na viongozi wengine wa Serikali kwa lengo la kuendeleza na kupanua ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
Ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Belarus pamoja na kukuza ushirikiano wa kiuchumi katika maeneo yenye maslahi ya pamoja.

.jpeg)


.jpeg)


No comments:
Post a Comment