Monday, April 13, 2026

RAIS DKT. MWINYI AWAAPISHA WAKUU WA WILAYA WAPYA IKULU ZANZIBAR

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewaapisha Wakuu wa Wilaya aliowateua hivi karibuni.

Hafla hiyo ya uapisho imefanyika leo tarehe 13 Aprili 2026, Ikulu Zanzibar, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama pamoja na wanafamilia wa Wakuu wa Wilaya walioapishwa.

Walioapishwa ni:

* Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A, Mhe. Lailah Burhani Ngozi

* Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Mhe. Dkt. Said Haji Mrisho

* Mkuu wa Wilaya ya Magharibi B, Mhe. Ali Abdalla Said Natepe

* Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini A, Mhe. Riziki Daniel Yussuf

* Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake, Mhe. Zuhura Mgeni Othman

Hafla hiyo imehudhuriwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla; Jaji Mkuu wa Zanzibar, Khamis Ramadhan Abdalla; Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi Talib Haji; Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kaabi; Wakuu wa Mikoa pamoja na baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.



No comments:

Makamu wa Rais Dkt. Nchimbi Aungana na Waombolezaji Chato Katika Ibada ya Kumuaga Mama wa Hayati Dkt. John Magufuli

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa na waombolezaji mbalimbali kushiriki Ibada ya kumu...