Thursday, June 26, 2025

RAIS SAMIA ASAFIRI KWENDA DODOMA KUHITIMISHA SHUGHULI ZA BUNGE LA 12








Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 26 Juni 2025, amesafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Jijini Dodoma kwa ziara rasmi ya kiserikali.

Safari hii inaambatana na tukio muhimu la kitaifa, ambapo kesho tarehe 27 Juni 2025, Mhe. Rais Dkt. Samia anatarajiwa kutoa hotuba maalum na kuhitimisha rasmi shughuli za Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hotuba ya Rais inatarajiwa kugusa masuala muhimu ya kitaifa ikiwemo tathmini ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo, mwenendo wa kisiasa na kijamii nchini, pamoja na mwelekeo wa Serikali katika kipindi kijacho. Tukio hili ni muhimu kwa taifa kwani linaweka msingi wa maelekeo mapya kwa mihimili ya dola, hasa Bunge na Serikali.

Wananchi wanaendelea kufuatilia kwa karibu matukio haya ya kihistoria ambayo yanadhihirisha uimara wa demokrasia na utawala bora nchini Tanzania chini ya uongozi wa Rais Samia.

No comments:

RAIS SAMIA ASAFIRI KWENDA DODOMA KUHITIMISHA SHUGHULI ZA BUNGE LA 12

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 26 Juni 2025, amesafiri kutoka Dar es Salaam kuelek...