Tuesday, June 03, 2025

MWENGE WA UHURU 2025 WAPONGEZA MIRADI YOTE WILAYA YA KIGAMBONI – HAKUNA MRADI ULIYOKATALIWA













Dar es Salaam, Juni 3, 2025
– Mwenge wa Uhuru 2025 umeendelea na mbio zake katika Mkoa wa Dar es Salaam, ambapo katika Wilaya ya Kigamboni umeweka historia kwa kupitisha miradi yote saba ya maendeleo iliyokaguliwa, bila kukataliwa hata mmoja.

Miradi hiyo saba, yenye thamani ya Shilingi 6,743,696,588.37, imekaguliwa kwa kina na Mwenge wa Uhuru na kupokelewa kwa pongezi kutokana na utekelezaji wake bora. Mwenge huo umefanya kazi mbalimbali ikiwemo kutembelea, kukagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi hiyo.

Baadhi ya miradi iliyotembelewa Kigamboni ni pamoja na:
✅ Ujenzi wa barabara ya Rombo Bar – RC Church yenye urefu wa km 0.39
✅ Ujenzi wa barabara ya Kivukoni – Shule ya Msingi yenye urefu wa km 0.25
✅ Mradi wa Kikundi cha Vijana "Umoja Kwanza"
✅ Ujenzi wa Kituo cha Afya Mjimwema
✅ Mradi wa mazingira: taka ngumu na nishati safi
✅ Mradi wa usambazaji wa maji
✅ Ukarabati na upanuzi wa Ofisi ya Serikali ya Mtaa Mwera
✅ Ujenzi wa bweni la wanafunzi – Shule ya Sekondari Kidete

Aidha, mafanikio haya ni ishara ya usimamizi madhubuti na utekelezaji makini wa miradi ya maendeleo kwa wananchi wa Kigamboni, sambamba na dhamira ya Serikali kuhakikisha huduma bora zinawafikia wananchi hadi ngazi ya chini.

Leo, Juni 3, 2025, Mwenge wa Uhuru unaendelea na mbio zake katika Wilaya ya Ilala, ambapo pia utatembelea, utakagua, utaweka jiwe la msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya hiyo.

Mwenge wa Uhuru – Kielelezo cha Uwajibikaji, Umoja na Maendeleo!

No comments:

Bodi ya TFS yatembelea Hifadhi za Pugu-Kazimzumbwi na Vikindu, yapongeza kasi ya uwekezaji wa utalii wa ikolojia

Na Mwandishi Wetu, Kisarawe – Pwani Ujumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) umetembelea Hifadhi za Mazingira ...