Na Mwandishi Wetu, Kondoa
Uingizaji wa mifugo kwenye pori la akiba la Mkungunero lililoko wilayani Kondoa mkoani Dodoma umeathiri uhifadhi wa pori hilo na kusababisha kukauka kwa baadhi ya vyanzo vya maji na kutoweka kwa baadhi ya wanyamapori adimu.
Meneja wa Pori la akiba la Mkungunero, Emmanuel Bilaso akizungumza na a waandishi wa habari waliotembelea pori hilo hivi karibuni amesema pori hilo linalopakana na Hifadhi ya Taifa ya Tarangire lina vyanzo muhimu vya maji ambayo yanayotegemewa na wananchi wengi kwa shughuli za kijamii na kiuchumi.
Bilaso amesema pori hilo la Mkungunero pia lina vyanzo vya maji ya mto Tarangire ambao ndiyo uhai wa Hifadhi ya taifa ya Tarangire na akatoa wito kwa wananchi kutilia mkazo uhifadhi ambao una umuhimu mkubwa kwa jamii na maendeleo ya taifa.
Amesema operesheni inayoendelea katika pori hilo imefanikisha kukamata kwa mifugo mingi katika pori hilo ambayo inachunga humo kinyume na sheria ya uhifadhi ambayo inakataza shughuli za binadamu kwenye maeneo yaliyohifadhiwa.
“Tumekamata ng’ombe zaidi ya 230 ambao waliingizwa na wananchi kinyume cha sheria na wamefikishwa mahakamani na kutozwa faini ya zaidi ya shilingi milioni 6” alisema bwana Bilaso.
Aliongeza kuwa kuingiza ng’ombe ndani ya hifadhi ni kinyume cha sheria ya uhifadhi ambayo inatoa adhabu kali ikiwemo kutaifisha mifugo inayokamatwa ili iwe fundisho kwa watu wanaovunja sheria za uhifadhi.
Nae Mkuu wa mkoa wilaya ya Kondoa Sezaria Makota amewaonya wananchi wanaingiza mifugo katika pori hilo kuacha mara moja vinginevyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao ili iwe fundisho kwa watu wanaovunja sheria na kuingiza mifugo kwenye maeneo yaliyohifadhiwa.
Amesema wilaya inaandaa mkakati wa uwepo wa makao makuu ya ncho Dodoma na kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya lami kutoka Dodoma mpaka Babati kuwa fursa ya kiuchumi kwa wananchi na taifa.
“Tuna vivutio vingi vya utalii likiwemo pori la akiba la Mkungunero na mapango yenye michoro ya kale, ni matarajio yetu kwamba viongozi wengi na wabunge watapata fursa ya kutembelea na hasa kwa sasa ambapo barabara ya lami kutoka Dodoma mpaka Babati imekamilika´alisema mkuu wa wilaya.
lenye wanyamapori wengi wakiwemo simba, tembo, nyati na mimea adimu meneja wa pori la akiba la mkungunero emmanuel bilaso amesema watuhumiwa waliokamatwa
Nao baadhi ya wananchi wanaoishi kwenye vijiji kuzunguka pori hilo wameiomba serikali kuweka vipaumbele katika uhifadhi wa pori hilo la akiba la Mkungunero ikiwemo kulipa fidia kwa baadhi ya wananchi wanaotakiwa kupisha uhifadhi endelevu wa pori kama tathimini ilivyofanywa na serikali kwa mujibu wa sheria.
Diwani wa kata ya Itaswi Said Mohamed Chobu alisema wananchi wanatambua umuhimu wa pori hilo lakini ni vizuri sasa wizara ya maliasili na utalii ikalipa fidia kwa wananchi kwenye vijiji kandokando ya hifadhi ili kuepuka uharibifu wa mazingira na migogoro baina ya wananchi na wahifadhi.
Comments