Friday, September 15, 2017

BANK OF AFRICA – TANZANIA yazindua program mpya ya kibenki ya “SWAHIBA MOBILE APP”

Sehemu ya wageni waalikwa wakiwa kwenye meza kuu.

Mkurugenzi Mtendaji wa BANK OF AFRICA – TANZANIA, Mr. Ammishaddai Owusu-Amoah akizindua rasmi program ya SWAHIBA Mobile App. Kulia kwake ni mkuu wa kitengo cha rasilimali watu wa benki hiyo Ms. Mercy Msuya na Meneja Masoko, utafiti na maendeleo wa benki hiyo ndg. Muganyizi Bisheko.

Mr. Emmanuel Mshindo, Mkuu wakitengo cha Huduma mbadala za kibenki akitoa maelezo juu ya huduma mbalimbali zipatikanazo katika program ya SWAHIBA Mobile, wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma hiyo mapema hii leo.

Mkurugenzi Mkuu wa MaxCom Africa, watoaji wa huduma za Max Malipo pichani ndugu Jameson Kasati, ameipongeza BANK OF AFRICA kwa hatua za makusudi za kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma zake za kibenki. Aidha aliongeza Zaidi kua mtazamo wa BANK OF AFRICA wa kutumia mabadiliko ya kiteknolojia na kidigitali katika kusogeza huduma zake karibu Zaidi kwa watanzania unashabihiana na wa MaxCom.

Naibu Mkurugenzi wa BANK OF AFRICA Bw. Wasia Mushi, akiongea na wageni waalikwa (hawapo pichani) katika hafla ya uzinduzi wa program ya SWAHIBA Mobile mapema hii leo.

Sehemu ya wageni waalikwa, uongozi na wafanyakazi wa BANK OF AFRICA wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya hafla ya uzinduzi rasmi wa Programu ya SWAHIBA Mobile.

BANK OF AFRICA – TANZANIA imezindua programu yake mpya ya kibenki inayoitwa "SWAHIBA Mobile" kwenye soko la Tanzania. Huduma hii inakuja kama muendelezo wa programu ya B- Mobile, inayoruhusu watumiaji kufurahia huduma kamili za kibenki kupitia aina yoyote ya simu za mkononi, wakati wowote.

SWAHIBA Mobile App inawapa wateja urahisi wa kutumia huduma za kibenki katika simu kwani inakuja na muonekano mzuri Zaidi na sifa nyingi mpya zinanzowarahisishia wateja kufuatilia akaunti zao za binafsi na za kibiashara kwa wakati mmoja.

Huduma zipatikanazo kwenye programu hii ni: huduma za kuhamisha fedha, huduma za hundi, maombi ya mkopo wa papo hapo, malipo ya bili mbalimbali, huduma za utoaji fedha kwenye ATM bila kadi, kuongeza muda wa maongezi, usajili binafsi wa mobile banking na huduma za e-chama pamoja na nyingine nyingi.

Zaidi ya hayo, SWAHIBA Mobile APP inaweza kutumiwa na Mtanzania yoyote hata ambae si mteja wa BANK OF AFRICA. Hii ni kupitia huduma mbalimbali zinazopatikana kabla ya kuingia kwenye program yaani “without Log in services”. huduma hizi ni kama vile maelezo kuhusu Huduma mbalimbali zitolewazo na BANK OF AFRICA, Maombi ya Mikopo, maelekezo kuhusu yalipo Matawi ya BANK OF AFRICA na ATMs, pamoja na viwango vya ubadilishaji fedha za kigeni.

Mr. Ammishaddai Owusu-Amoah, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa BANK OF AFRICA - TANZANIA alisema Benki yake inajivunia kuanzisha programu hii mpya ya benki kiganjani katika wakati huu muhimu ambapo benki hiyo inaadhimisha miaka 10 ya biashara katika nchi ya Tanzania. "Uzinduzi wa SWAHIBA Mobile App ni namna ya kipekee ya kuwasilisha shukrani zetu kwa wateja, jamii, washirika, wamiliki na wadau wote, walio tupa ushirikiano wa kutosha katika kipindi cha miaka 10 ya kazi nchini ".

"Huduma hii pia inakuja kutia msistizo wa ahadi yetu ya kuweka mapendekezo ya wateja wetu kwanza na kuwaongezea uzoefu wa kidigitli Zaidi katika ukuwaji wa sayansi na technologia. Mkurugenzi aliendelea kueleza “Pia inathibitisha uamuzi wa benki wa kujenga uwepo wake wa kidigitali na kukidhi mahitaji ya haraka ya wateja wetu "

Bwana Emmanuel ameeleza: " katika dunia ya sasa kuna ongezeko kubwa sana la matumizi ya technologia pamoja na matumizi ya “Simu za kisasa na Tablets” tumeunda huduma hii katika ubunifu na uwezo wa hali ya juu sana na ambao mtanzania yoyote anaweza kutumia. Program hii inamuongezea mteja uzoefu wa kubenki kidigitali Zaidi huku akifurahia huduma maridhawa kwa uharaka zadid bila kujali kuhusu foleni benki au kufungwa kwa tawi.

Mbali na ongezeko la huduma SWAHIBA Mobile App inamfumo bora wa ulinzi wa fedha. “ Ulinzi wa fedha za wateja wetu ni kitu cha kwanza kabisa ambacho benki inaangalia kwenye programu hii benki imeingiza vipengele vya usalama wa hali ya juu kama vile vinavyopatikana kwenye benki ya mtandao (B WEB SMART) "alieleza Mr. Mshindo.

“Program yetu hii ni rahisi sana kutumia ikiwa imeundwa kwa kumzingatia mteja ili kumwezesha kuona machaguo mbalimbali punde tuu anapifungua program hii na hili limefanyika ili kupunguza mlolongo mrefu katika uchaguzi wa huduma ambayo mteja atakua anahitaji” alisema Mshindo, kwa sasa SWAHIBA MOBILE App, inaweza kupakuliwa kupitia “ Play store” kwa watumiaji wa Android na Apple iOS kwa watumiaji wa Iphone.

No comments: