Dkt. Mwakyembe Azindua Mpango wa Usajili na Utoaji Vyeti kwa Watoto waliochini ya Umri Miaka Mitano kwa Mtwara na Lindi
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na Wakazi wa Wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara (hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa Usajili na Utoaji Vyeti kwa Watoto waliochini ya Umri Miaka Mitano kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akikata utepe katika Kitabu cha Usajili pamoja na Simu kuashiria Uzinduzi wa Mpango wa Usajili na Utoaji Vyeti kwa Watoto waliochini ya Umri Miaka Mitano kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara .
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na Wadau mbalimbali wanaosaidia Mpango wa Usajili na Utoaji Vyeti kwa Watoto waliochini ya Umri Miaka Mitano mara baada ya kuuzindua Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, 26 Septemba, 2017.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (aliyevaa kofia ya pama) akiwakabidhi vyeti Wazazi kwa niaba ya watoto wao wenye umri chini ya miaka mitano wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa Usajili na Utoaji Vyeti kwa Watoto waliochini ya Umri Miaka Mitano jana Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara 26 Septemba, 2017.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM
………………
Na Benedict Liwenga-WHUSM.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. John Palamagamba amezindua Mpango wa Usajili na Utoaji Vyeti kwa Watoto waliochini ya Umri Miaka Mitano kwa Mikoa ya Mtwara na Lindi.
Uzinduzi huo umefanyika leo katika Viwanja vya Matogolo Wilayani Tandahimba Mkoani Mtwara ukiwa na lengo la kuwasajili watoto waliochini ya umri miaka mitano pamoja na kuwapatia vyeti ambavyo vitawasaidia kutambulika kwao na kisha kupewa nyaraka za uthibitisho yaani vyeti vya kuzaliwa.
Waziri Mwakyembe amesema kwamba, katika kupanga maendeleo ya nchi kunahitajika takwimu sahihi za matukio muhimu za Watanzania ambazo zinaelezea taarifa zao za kuzaliwa ikiwemo za vifo kwakuwa takwimu hizo zinasaidia kujua mahitaji ya wananchi katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, lishe pamoja na sehemu nyinginezo.
“Mpango huu utaondoa utegemezi wa takwimu za kuhisia, takwimu za kukadilia ndugu zangu mfumo tulionao sasa unategemea Sensa ambayo hufanyika kila baada ya miaka 10, na matukio bado yanatokea, hivyo kutumia Mpango huu kutasaidia kupata takwimu sahihi na halisi za Watanzania wote”, alisema, Dkt. Mwakyembe.
Ameongeza kuwa, Mikoa ya Lindi na Mtwara itanufaika na mpango huo kwakuwa Serikali itakuwa inatambua mahitaji halisi ya wananchi kupitia taarifa zitakazochukuliwa za uandikishaji wa watoto hao, huku akisisitiza kuwa, anaamini kwamba mikoa hiyo itakuwa chachu ya kuongezeka kwa idadi ya watoto watakaoandikishwa kama ilivyofanyika katika baadhi ya mikoa mingine ya Tanzania.
Comments