RC MAKONDA KUKABIDHIWA MAGARI 18 YA POLISI KATI YA 26 YALIYOPELEKWA MOSHI KUKARABATIWA


Askari Pilisi wakiwa tayari kwa kazi katika moja ya magari 18 yaliyokamilika kwa ukarabati kati ya magari 26 yaliyopelekwa kwenye Gereji la RSA mjini Moshi na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda kwa matengenezo makubwa wakati alipoyakagua leo mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akikagua moja ya magari 18 kati ya 26 ya polisi Dar es salaam yaliyopelekwa mjini Moshi katika Gereji ya RSA kwa matengenezo makubwa Mkuu wa mkoa huya ameyakagua magari hayo na atakabidhiwa magari 18 ambayo yamekamilika.
Baadhi ya magari ambayo tayari yamekamilika kwa matengenezo.



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda jana  ametembelea na kukagua Ukarabati wa Magari 26 ya Polisi yaliyopelekwa Mkoani Kilimanjaro yakiwa Mabovu kwaajili ya kukarabatiwa na kubadilishwa Mwonekano ambapo hadi sasa Magari 18 yapo hatua ya mwisho kukamilika.

Magari hayo ambayo yalipelekwa Moshi yakiwa Chakavu kwa sasa baadhi yanatembea ambapo yamepakwa Rangi huku yakifungwa vifaa mbalimbali ikiwemo Magurudumu Mapya, Taa,Vioo,Bodi, Side Mirrow na vifaa vingine muhimu.

Makonda amesema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa na kusema kuwa atakabidhiwa Magari hayo mwanzoni mwa mwezi October ili ayakabidhi kwa Jeshi la Polis.Amesema Magari hayo yenye mwonekano kama yale ya UN yatakuwa na uwezo wa kubeba Askari Tisa nyuma wakiwa wamekaa ambapo Watatu watakuwa wakitazama Nyuma, Watatu Kushoto, Watatu Kulia na Mmoja Mbele wote wakiwa wamebeba silaha.

Aidha Makonda amesema kupatikana kwa Magari hayo yatasaidia kupunguza vitendo vya Uhalifu kwa Wananchi.RC Makonda amesema kuwa lengo lake ni kuona hakuna Mwananchi yoyote anaeibiwa au kuporwa kitu.

Hata hivyo amesema Baadhi ya Askari walikuwa wakipoteza maisha na kuporwa Silaha kutokana na aina ya Magari waliyokuwa wakitumia kutowapa uwezo wa kukabiliana na wahalifu hivyo Magari hayo yatamaliza matukio hayo.

Ameishukuru kampuni ya RSA Limited kwa kumuunga mkono kwa kujitolea kukarabati Magari 56 ya Jeshi la Polisi kwa kuyafanya kuwa ya kisasa na Mapya.Sanjari na hayo amesema Magari hayo yataenda kufanya Doria kwa masaa 24.

Nae Mkurugenzi wa Kampuni ya RSA Bwana Manmohan Bhamra amesema kwa sasa Magari hayo ni sawa na Mapya kwakuwa yamewekwa vifaa vipya.
Amesema Magari yote watayakabidhi kwa wakati iliyakaongeze tija katika kuimarisha Ulinzi na Usalama kwa Wananchi.

Comments