ELVAS MUSIBA AFARIKI DUNIA!


Hayati Elvis Musiba.

Aliyekuwa Rais wa Chama Cha Wafanyabiashara na Wenye Viwanda nchini Tanzania (TCCIA), Elvis Musiba, amefariki dunia leo jijini Dar es salaam. kwa mujibu wa taarifa fupi iliyotolewa na ITV jioni hii, taarifa kamili na mipango ya mazishi itatolewa baadae na msiba uko nyumbani kwa marehemu, Mikocheni. Kwa wapenzi wa hadithi za vitabu, watamkumbuka marehemu kwa zile novo zake maarufu za Kikosi Cha Kisasi cha Willy Gamba na Njama zilizotamba nchini Tanzania katika miaka ya 80. Mungu alilaze roho ya marehemu peponi - Amin!

Comments

emu-three said…
Mungu ailaze mahala pema peponi. Huyu ni mmoja aliyekuwa akinivutia katika vitabu vyeka vya `kufa na kupona nk.' baadaye nilipomsoma Jamles Hadley chase, nikamsahau.
Kwake yeye kafa kiwiliwili lakini kimawazo tutakuwa naye kwani najua bado vitabu vyake vipo kwenye chati!
Unknown said…
Mungu na ailaze roho ya marehemu pema peponi. Tutamkumbuka kwa ushujaa wake wa ki-Willy Gamba kwa kutuletea burudani tamu hasa kwa sisi ambao enzi hizo tulikuwa ni vijana wadogo na kwa kusoma vitabu vyake ilitusaidia sana kupanua mawazo yetu. Amen
Anonymous said…
aisee huyu baba alikuwa mtunzi sn maana hicho kitabu nimevuma sana kwani tumekisikia sn na stori zake ni nzuri mno mungu amlaze mahali pema peponi amen.

marimar

Popular posts from this blog

JESHI LA MAGEREZA NCHINI WAJADILIANA NA NHC NAMNA YA KUENDELEZA MAKAZI MAKAO MAKUU DODOMA

Baraza Jipya la Mawaziri