Ujumbe wa Tanzania waondoka kwenda Miss World


Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania,Ankal Hashim Lundenga akiwa katika mazungumzo na wazazi wa Genevieve Emmanuel mrembo anaeiwakilisha Tanzania katika masindano ya Dunia,katika uwanja wa ndege wa J.K. Nyerere leo.

Ujumbe wa watu 5 ukiongozwa na Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania bw. Hashim Lundenga umeondoka nchini leo kuelekea Sanya China katika kuhudhuria mashindano ya urembo ya dunia yaliyopangwa kufanyika Jumamosi Tarehe 30 Oktoba 2010.

Katika ujumbe huo yupo pia Katibu Mkuu wa Kamati bw. Bosco Majaliwa, Miss Tanzania Mshindi wa 2 Glory Mwanga, na Miss Temeke mshindi wa 2 Anna Daudi ambaye pia alifanikiwa kuingia katika 10 bora ya Fainali za Miss Tanzania 2010.

Mama Mzazi wa Miss Tanzania 2010 Genevieve Emmanuel, Mrs. Mary E. Mpangala pia yumo katika msafara huo ili kushuhudia Fainali hizo za kumtafuta Mrembo wa dunia ambazo zitafanyika Jumamosi hii katika kisiwa cha Hainan huko Sanya China.

Msafara huo unatarajia kurejea nchini Tarehe 3 Novemba 2010.

Comments