Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Oliver Mhaiki (kulia) wakitiliana saini mkataba wa ujenzi wa majengo ya kudumu ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) na Meneja Mkuu wa Kampuni ya ujenzi ya BCEG ya China Bw. Jia Jianhui mara baada ya kutiliana saini makataba huo jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Oktoba 18, 2010). Katikati ni Afisa kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Benas Mayogu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Oliver Mhaiki (katikati) akibadilishana mkataba wa ujenzi wa majengo ya kudumu ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) na Meneja Mkuu wa Kampuni ya ujenzi ya BCEG ya China Bw. Jia Jianhui mara baada ya kutiliana saini makataba huo jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Oktoba 18, 2010). Kulia ni Kaimu Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Gerald Ndika.
Picha zote na Mohammed Mhina.
Wizara ya Katiba na Sheria leo imetiliana saini na kampuni ya Beijing Construction Engineering Group Company Ltd kutoka China kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya kudumu ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST).
Ujenzi huo wenye thamani ya aidi ya shilingi bilioni 16 unafanyika jijini Dar es Salaam kupitia Programu ya Maboresho ya Sekta ya Sheria (LSRP) kwa thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 16.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya utiaji saini, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Oliver Mhaiki alisema ujenzi huo unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 15.
Katibu Mkuu huyo aliitaka kampuni hiyo kuhakikisha kuwa ujenzi huo unakamilika kwa wakati na kiwango kama ilivyokusudiwa ili kuondokana na changamoto zinazoikumba Taasisi hiyo kutokana na kutokuwa na majengo ya kudumu.
Kwa sasa Taasisi hiyo inaendesha mafunzo yake kwa kutumia majengo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati ikisubiri ujenzi wa majengo yake ukamilike.
Akiongea katika hafla hiyo fupi, Kaimu Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Gerald Ndika alisema ujenzi huo unatarajiwa kujumuisha majengo ya kisasa vikiwemo vyumba vya madarasa, maktaba, nyumba za watumishi, hosteli na vyumba vya mahakama vya mazoezi.
“Hii itaifanya taasisi kutoa mafunzo ya vitendo kwa wahitimu wa shahada ya kwanza ya sheria sheria kwa ufanisi zaidi na hivyo kutimiza ile azma ya kutoa mafunzo sahihi ya vitendo,” alisema Dkt. Ndika.
“Baada ya kukamilika, wanafunzi wetu wataruhusiwa kutoa huduma za kisheria Mahakamani kwa wateja chini ya usimamizi wa wanasheria wazoefu,” alisema za Dkt. Ndika na kuongeza kuwa udahili wa wanafunzi unatarajiwa kuongezeka kutoka wastani wa 300 wa sasa hadi 1,000 kwa mwaka, alisema.
Comments