Hayati Elvis Musiba.
Aliyekuwa Rais wa Chama Cha Wafanyabiashara na Wenye Viwanda nchini Tanzania (TCCIA), Elvis Musiba, amefariki dunia leo jijini Dar es salaam. kwa mujibu wa taarifa fupi iliyotolewa na ITV jioni hii, taarifa kamili na mipango ya mazishi itatolewa baadae na msiba uko nyumbani kwa marehemu, Mikocheni. Kwa wapenzi wa hadithi za vitabu, watamkumbuka marehemu kwa zile novo zake maarufu za Kikosi Cha Kisasi cha Willy Gamba na Njama zilizotamba nchini Tanzania katika miaka ya 80. Mungu alilaze roho ya marehemu peponi - Amin!
Comments
Kwake yeye kafa kiwiliwili lakini kimawazo tutakuwa naye kwani najua bado vitabu vyake vipo kwenye chati!
marimar