Monday, August 18, 2008

Rais apoke ripoti ya Epa kimyakimya


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea rasmi ripoti ya uchunguzi kuhusu upotevu wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Nje(External Payments Account–EPA)kutoka kwa Mwenyekiti wa Timu iliyofanya uchunguzi huo,Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Johnson Mwanyika katika halfa fupi iliyofanyika leo(Jumatatu,Agosti 18,2008)Ikulu,Dar Es salaam.Wengine katika picha ni wajumbe wa timu iliyofanya uchunguzi huo,Mkuu wa jeshi la polisi nchini,Saidi Mwema na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa nchini Dr.Edward Hosea.Picha na Freddy Maro/Ikulu

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiipitia ripoti ya uchunguzi kuhusu upotevu wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Nje(External Payments Account-EPA)muda mfupi baada ya kukabidhiwa na mwenyekiti wa timu iliyoongoza uchunguzi huo Mwanasheria Mkuu Wa Serikali Johnson Mwanyika.Wengine katika timu hiyo ni Mkuu wa Jeshi la polisi nchini Saidi Mwema na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa nchini Dr.Edward Hosea.Ripoti hiyo ilikabidhiwa kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo hii.

1 comment:

Anonymous said...

Yahya, hivi mlitaka apokee kwa matarumbeta? Ama iwe ni siku ya mapumziko ahutubie wananchi? Mbona mnakuwa too cynical? Kikubwa hapa ni jinsi atakavyoshughulikia ripoti na si style ya mapokezi.