Hatimaye Chacha Wangwe azikwa



ALIYEKUWA Mbunge wa Tarime (Chadema), Chacha Wangwe amezikwa jana kwenye makaburi ya kijijini kwao Kimakorere baada ya familia kuridhika na uchunguzi wao uliofanyika na daktari wao.

Wangwe alizikwa jana majira ya saa 12 jioni huku kukiwa na hali tata, wakati baadhi ya ndugu wakigoma na wengine kukubali.

Mazishi hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa nchini ambao pia walikuwapo katika uchunguzi uliofanyika kabla.

Akizungumza kabla ya mazishi kwa niaba ya familia muda mfupi baada ya kutoka ndani ya chumba cha uchunguzi, Prof Samwel Wangwe alisema jana kuwa uchunguzi walioutaka familia umekamilika na kwamba sasa wameridhika kuwa mbunge huyo alikufa kwa ajali na si vinginevyo. Habari ya Fredrick Katulanda.

Comments