Friday, August 01, 2008

Watoto wagomea nauli mpya



MAMIA ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari jijini Dar es Salaam jana waliandamana hadi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro kupinga ongezeko la nauli yao kutoka Sh50 hadi Sh100.

Wanafunzi hao walihoji sababu za serikali kuwaongezea nauli wakati imeshindwa kuwafilisi watuhumiwa wa ufisadi na kutumia fedha walizoiba kununua magari kwa ajili yao.

Katika maandamano hayo yaliyoanza majira ya saa 5:00asubuhi wanafunzi hao wakiwa na mabango walipinga kulipa nauli hiyo na kushinikiza serikali iwakubalie waendelee kulipa Sh50.

Baadhi ya mabango yalisomeka: "Wafilisiwe Chenge, Mkapa, Karamagi na Yona tuletewe mabasi ya shule, J.K utawala umekushinda, Tulipe Sh100 kwa lipi uliloboresha?".

1 comment:

Anonymous said...

Aanzaye kwa uluzi mwisho ataimba! Wameanza wanafunzi halafu wafuatie wazazi.