
Katika tukio lililojaa hamasa na uzalendo wa kitaaluma, baadhi ya wafanyakazi walionekana wakigongeana glasi kwa bashasha kama ishara ya kusherehekea mafanikio hayo makubwa ya kimkakati. Tukio hilo liliambatana na furaha ya mafanikio, ubunifu, na dhamira ya kampuni hiyo kuendelea kuwa kioo cha jamii na kinara wa habari za kuaminika nchini.
Sura mpya ya gazeti la Mwananchi inatajwa kuwa ya kisasa zaidi, yenye mvuto wa kimtazamo na urahisi wa kusoma, ikilenga kukidhi mahitaji ya wasomaji wa leo katika enzi ya kidijitali na ushindani mkubwa wa habari.
Katika picha iliyopigwa na Fidelis Felix, wafanyakazi hao walionekana wakiwa na nyuso za furaha – ushahidi tosha wa ari mpya ndani ya taasisi hiyo kongwe ya habari nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment