Thursday, May 08, 2014

MULT CHOICE TANZANIA(DSTV) WAZINDUA KING’AMUZI KIPYA AINA YA EXPLORER

Wadau na wateja wa DSTV wakijadiliana jambo na Meneja uendeshaji Ronald Shelukindo wakati wa uzinduzi wa king’amuzi chao kipya aina ya explorer
Wageni waalikwa na wateja wa DSTV wakibadilishana mawazo ndani ya ukumbi wa Southern Sun Hotel jana kwenye uzinduzi wa king’amuzi kipya aina ya Explorer
Edo Kumwembe akiuliza jambo kwa Meneja mahusiano wa DSTV Barouba Kambogi  wa nne kutoka kushoto jana kwenye Hotel ya Southern Sun
 Wateja na wadau wa DSTV wakiwa wanabadilishana mawazo kuhusu huduma mpya iliyoanzishwa na DSTV ya king’amuzi kipya aina ya Explorer
 Wa pili kutoka kushoto ni Meneje wa uendeshaji DSTV Bwana Ronald Shelukindo na Meneja mahusiano Barba Kambogi wakifuatilia maelekezo kutoka kwenye screen kubwa(haipo pichani)kuhusu mapinduzi yaliyofanya toka miaka ya 1950 mpaka leo kwenye teknolojia ya urushaji wa matangazo.
 Meneja uendeshaji mwenye shati ya kaki Ronald Shelukindo akifurahia jambo na Meneja uhusiano DSTV Barba Kambogi kwenye uzinduzi wa king’amuzi kipya aina ya explorer
 Meneja mahusiano wa DSTV Barba Kambogi akifafanua jambo kwa wateja wa DSTV jana
 Wateja wa DSTV wakifuatilia kwa umakini mkubwa uzinduzi wa king’amuzi kipya aina ya explorer
Meneja uendeshaji Ronald Shelukindo akifafanua utofauti wa king’amuzi hicho kipya na kile cha zamani jana Kwenye Hotel ya Southern Sun
Wanahabari wakichukua matukio kwa umakini kabisa
 Meneja uendeshaji Ronald Shelukindo akionyesha jinsi king’amuzi kipya aina ya explorer kinavyoweza kurekodi matukio tofauti na kuweza kuyaangalia baadae
Na DJ SEK BLOG

RAIS JAKAYA KIKWETE AUNDA TUME YA UCHUNGUZI MWENENDO WA OPERESHENI TOKOMEZA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameunda Tume ya Uchunguzi (Commission Inquiry) Kuhusu Vitendo vilivyotokana na Uendeshaji wa Operesheni Tokomeza.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar Es Salaam jion, Ijumaa, Mei 2, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Rais ameunda Tume hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 3 cha Sheria ya Uchunguzi Sura ya 32.
Kutokana na hatua yake ya kuunda Tume hiyo, Rais Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji na Balozi Mstaafu Hamisi Amiri Msumi kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo.
Aidha, Rais Kikwete amewateua Mheshimiwa Jaji Mstaafu Stephen Ernest Mtashiwa Ihema na Mheshimiwa Jaji Mstaafu Vincent Kitubio Damian Lyimo kuwa Makamishna. Rais pia amemteua Ndugu Frederick Manyanda, Wakili wa Serikali katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa Katibu wa Tume hiyo.
Taarifa ya Balozi Sefue imeongeza kuwa uteuzi huu ulianza, Alhamisi, Mei  2014.

UTEUZI WA MTENDAJI MKUU WA MAMLAKA YA UDHIBITI NA UNUNUZI WA UMMA (PPRA)

Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt Laurent M. Shirima kuwa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Ununuzi wa Umma (PPRA).

Dkt. Shirima ni Mkurugenzi wa kujenga Uwezo wa Huduma za Ushauri (Capacity Building and Advisory Service-PPRA) na pia ndiye anaye kaimu nafasi ya Mtendaji Mkuu wa PPRA.

Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Uteuzi huu umeanza tarehe 2 Mei, 2014.

Imetolewa na;

Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu-Dodoma
Tanzania.

6 Mei, 2014

Wednesday, May 07, 2014

Waumini wa dini ya kiislamu wakibeba jeneza lenye mwili wa Sheikh Hassan Ilunga kabla ya kumzika katika Makaburi ya Mwinyimkuu, Magomeni jijini Dar es Salaam


Waumini wa dini ya kiislamu wakibeba jeneza lenye mwili wa Sheikh Hassan Ilunga kabla ya kumzika katika Makaburi ya Mwinyimkuu, Magomeni jijini Dar es Salaam. Picha na Joseph Zablon 

Serikali inatarajia kuanza kutoa huduma za awali (interim services) katika mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) Kutoka Kimara mwisho hadi Kivukoni jijini Dar es Salaam mwaka 2015 baada ya miundombinu kukamilika

  Meneja Uhusiano Mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART) Bw. William Gatambi (kushoto) akiwaeleza  waandishi wa habari  Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo kuhusu  maendeleo ya mradi huo ambao awamu ya kwanza itakamilika mwishoni wa mwaka huu. Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Frank Mvungi
Meneja uendeshaji wa DART  Bw.Peter Munuo  akieleza kwa waandishi wa habari kuhusu faida za mradi  huo ikiwemo kuondoa tatizo la foleni katika jiji la Dar es salaam na viunga vyake.mara  mradi huo  utakapoanza mapema mwakani


  Meneja usimamizi wa Barabara toka Wakala wa mabasi yaendayo haraka (DART) Mhandisi Mohamedi Kaganda (kulia) akielezea kwa waandishi wa Habar (hawapo pichani)  Jijini Dar Es Salaam namna mabasi hayo yatakavyofanya safari zake mara  awamu ya kwanza ya mradi huo itakapoanza mapema mwakani , Kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Frank Mvungi.Picha na Georgina Misama
---
Na Frank Mvungi- Maelezo
Serikali inatarajia kuanza kutoa huduma za awali (interim services) katika mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) Kutoka Kimara mwisho hadi Kivukoni jijini Dar es salaam mwaka 2015 baada ya miundombinu kukamilika.
Hayo yamesemwa na Meneja Uhusiano wa Wakala wa mabasi yaendayo haraka (DART) Bw.William Gatambi  wakati wa mkutano na waandishi wa habari  jijini Dar es salaam.
Gatambi alisema kuwa mara baada ya kukamilika kwa miundo mbinu ya mradi huo awamu ya kwanza mwishoni mwa mwaka 2014 itasadia kufanikisha usafiri wenye tija kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake.
Miundombinu hiyo, inajumuisha barabara ya kilomita 20.9 kuanzia Kimara Mwisho hadi Kivukoni,Barabara ya Kawawa kutoka Morocco hadi Magomeni na Barabara ya Msimbazi hadi eneo la Gerezani Kariakoo.
 Aliongeza kuwa ina vituo vidogo 27,vituo vikuu vitano, vituo mlisho vine na karakana mbili. Pia inajumuisha njia za waenda kwa miguu na baiskeli.
Akifafanua Gatambi alisema mradi wa majaribio utaanza na mabasi 20 yatakayokuwa na uwezo wa kuchukua abiria kati ya 145 hadi 160 kwa wakati mmoja hali itakayosaidia kuondoa kabisa kadhia ya usafiri kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam.
Aidha, katika mradi huo wa majaribio Gatambi amesema kutakuwa na mabasi mengine 10 yenye uwezo wa kuchukua abiria kati ya 50 na 60 ambayo yatatumika kuchukua abiria kutoka pembezoni mwa jiji la Dar es salaam kuja katika vituo vikuu vya mabasi yaendayo Haraka.
Kwa upande wakeMeneja Usimamizi wa Barabara wa DART Mhandisi Mohamed Kuganda amesema mradi huo utasaidia kuondoa tatizo la foleni Jijini Dar es salaam na kuwafanya wananchi kupata huduma ya usafiri yenye kukidhi viwango vya Kimataifa.
Pia Kuganda alisema DART kwa kushirikiana na Halmashauri za Jiji la Dar es salaam inafanya maandalizi ya kuboresha barabara mlisho (feeder roads) katika maeneo yatakayotumiwa na mabasi mlisho.

Katika mradi wa mabasi yaendayo haraka kutakuwa na Vituo Vikuu (terminals) vitano 5 katika, maeneo ya Kimara, Ubungo, Morocco, Kariakoo na Kivukoni ambapo vituo hivi ndiko mabasi yatakapokuwa yanaanzia na kumalizia safari kubadilishana abiria kati ya njia kuu na njia mlisho (feeder roads) ambapo vituo hivyo vikubwa vinatoa nafasi ya kuweza kuanzishwa kwa huduma muhimu kwenye vituo hivyo kama maeneo ya kukatia tiketi na vyoo.

Tuesday, May 06, 2014

JAJI BOMANI‏: ANDIKENI HABARI ZA KUMKOMBOA MWANANCHI

 Mshehereshaji ambaye ni Mwanakamati ya maandilizi ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014, Usia Nkhoma Ledama akiwatambulisha baadhi ya waandishi wa habari wakongwe (hawapo pichani) kwa mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mark Bomani.(Picha zote na Zainul Mzige).
DSC_0171
Baadhi ya waandishi wa habari wakongwe (Ma-veterans) wakimsalimia mgeni rasmi.…
Mshehereshaji ambaye ni Mwanakamati ya maandilizi ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014, Usia Nkhoma Ledama akiwatambulisha baadhi ya waandishi wa habari wakongwe (hawapo pichani) kwa mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mark Bomani.(Picha zote na Zainul Mzige).
DSC_0171
Baadhi ya waandishi wa habari wakongwe (Ma-veterans) wakimsalimia mgeni rasmi.
DSC_0077
Meza Kuu, kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Elimu, Sayansi na Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa (UNESCO) Bw. Abdul Wahab Coulibaly, Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) Bw. Ernest Sungura, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Bw. John Mongela, Mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mark Bomani, Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Bw. Mohamed Tibanyendera, Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Kenneth Simbaya na Meneja Utafiti na Ushapishaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. John Mirenyi.
DSC_0348
Mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mark Bomani, akitoa risala wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014 yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC jijini Arusha mwishoni mwa juma.
DSC_0429
Sehemu ya wadau wa tasnia ya Habari wakisikiliza risala ya mgeni rasmi.
DSC_0329
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Bw. John Mongela akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa wa Arusha kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika jijini Arusha kenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC.
DSC_0112
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Bw. Mohamed Tibanyendera, akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014 yaliyofanyika kwenye ukumbi wamikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha.
DSC_0163
Wageni waalikwa na wadau wa tasnia ya habari wakiwa kwenye ukimya kumkumbuka Mwandishi aliyeuwawa mkoani Iringa Daudi Mwangosi.
DSC_0188
Mkurugenzi wa Shirika la Elimu, Sayansi na Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa (UNESCO) Bw. Abdul Wahab Coulibaly, akitoa Ujumbe wa Pamoja wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Irina Bokovas kuhusiana na Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014.
DSC_0217
Meneja Machapisho, Utafiti na Uhifadhi Hati wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. John Mirenyi, akitoa maelezo ya machapisho mbalimbali yaliyoandaliwa na baraza hilo yakiwemo yenye madhila mbalimbali yaliwahi kuwakumba baadhi ya waandishi wa habari ndani na nje ya nchi.
DSC_0241
Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) Bw. Ernest Sungura, akizungumzia mchango wa mfuko huo unaowawezesha waandishi wa habari kutafuta habari za uchunguzi na zinazoigusa jamii.
DSC_0247
Wasanii wa Bendi ya Mrisho Mpoto (Mjomba Band) wakitoa burudani kwa wageni waalikwa wakati wa maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014 yaliyofanyika jijini Arusha mwishoni mwa juma.
DSC_0156
Sehemu ya wadau wa tasnia ya habari wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini hapo.
DSC_0259
Katibu wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT), Henry Muhanika, akisoma hotuba kwa niaba ya Dr. Reginald Mengi kwenye maadhisho hayo.
DSC_0269
Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Kenneth Simbaya, akizungumzia wakati wa maadhimisho hayo.
DSC_0286
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda, akizungumzia changamoto mbalimbali zinazowakumba waandishi wa habari wakati maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014 yaliyofanyika jijini Arusha.
DSC_0288
Mkurugenzi wa TAMWA, Bi. Valerie Msoka, akizungumzia changamoto za usawa wa Kijinsia katika uongozi kwenye Vyombo vya Habari nchini.
DSC_0304
Meneja Uhusiano wa TANAPA, Pascal Shelutete, akizungumzia ushiriki wao kwenye Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014 ambapo aliwataka waandishi wahabari kutumia kalamu zao vizuri katika kukuza Utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi.

RIDHIWANI KIKWETE NA GODFREY MGIMWA WAAPISHWA


Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda na watendaji wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya shughuli za Bunge kuanza leo Mei 6, 2014.
Mbunge Mpya wa Jimbo la Kalenga,Mh. Godfrey Mgimwa akisindikizwa na wabunge wa CCM kuingia Bungeni mjini Dodoma leo Mei 2014.
Mbunge Mpya wa Jimbo la Kalenga,Mh. Godfrey Mgimwa akila kiapo Bungeni mjini Dodoma leo Mei 6, 2014.
Mbunge Mpya wa Jimbo la Chalinze,Mh. Ridhiwani Kikwete akisindikizwa na wabunge wa CCM kuingia kwenye Ukumbu wa Bunge Mjini Dodoma, leo Mei 6, 2014
Mbunge Mpya wa Jimbo la Chalinze,Mh. Ridhiwani Kikwete akila kiapo Bungeni Mjini Dodoma,leo Mei 6, 2014.
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akimpongeza Mbunge Mpya wa Chalinze,Ridhiwani Kikwete baada ya kuapishwa, Bungeni Mjini Dodoma leo Mei 6, 2014.
Waziri wa Nchi,Sera na Uratibu wa Bunge,Mh. William Lukuvi akimpongeza Mbunge Mpya wa Chalinze,Ridhiwani Kikwete baada ya kuapishwa, Bungeni Mjini Dodoma leo Mei 6, 2014.
Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akiwa Bungeni Mjini Dodoma Mei 6,2014 wakati mwanae,Ridhiwani Kikwete alipoapishwa . Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema nchimbi.
Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete na familia wakiwa Bungeni Mjini Dodoma leo Mei 6,2014 wakati mwanae,Ridhiwani Kikwete alipoapishwa . Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma , Dr. Rehema Nchimbi.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NMB YATOA SOMO LA KUJENGA MITAJI, YAHIMIZA AKIBA YENYE MALENGO

  DODOMA. Benki ya NMB imewataka Watanzania kujenga utamaduni wa kuweka akiba kwa malengo na kufanya maamuzi sahihi ya uwekezaji ili kuimari...