Wednesday, January 04, 2017

MAMIA WAMUAGA RUBANI WA MARAIS, MBOWE AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA


Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akiongoza waombolezaji kuaga mwili wa marehemu Kenan Mhaiki Rubani Mstaafu wa ndege za marais wa Tanzania wakati wa shughuli ya kuaga mwili wake iliyofanyika Kunduchi, jijini Dar es Salaam Januari 2 2017. Mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda Songea Mjini Mkoani Ruvuma kwa mazishi yanayotayarajiwa kufanyika leo Januari 4, Makaburi ya Matogoro. (Imeandaliwa na Robert Okanda blogspot)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Leonard Chamriho akitoa salamu kwa niaba ya serikali wakati wa ibada ya misa na shughuli ya kumuaga marehemu Kenan Paul Mhaiki. 

Katibu Mkuu Kiongozi wa zamani, Balozi Ombeni Sefue akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Kenani Mhaiki Rubani Mstaafu wa ndege za marais wa Tanzania wakati wa shughuli ya kuaga mwili wake iliyofanyika Kunduchi, jijini Dar es Salaam. Mwili wa marehemu umesafirishwa jana kwenda Mkoani Ruvuma kwa mazishi yanayotayarajiwa kufanyika Januari 4 2017. soma zaidi hapa
Post a Comment