DIT KUZALISHA WATU WENYE UJUZI KWA AJILI SEKTA YA VIWANDA

Mkuu wa Taasisi ya DIT, Profesa Preksedis Ndomba akizungumza na waandishi wa habari juu ya mafunzo wanayotoa katika taasisi hiyo na umuhimu wa ushiriki katika uchumi wa viwanda leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Taasisi ya DIT, Profesa Preksedis Ndomba na Mkurugenzi wa Ajira wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera ,Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Ally Msaki wakisaini makubaliono ya Mafunzo kwa vijana 1000 katika Chuo cha DIT Mwanza.
Mkuu wa Taasisi ya DIT, Profesa Preksedis Ndomba akibadilishana hati za makubaliano na Mkurugenzi wa Ajira wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera ,Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Ally Msaki leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya waandishi habari wakiwa katika mkutano huo.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam DIT, imesema kuwa katika kufikia uchumi wa viwanda lazima vijana waandaliwe kwa ujuzi wa kuweza kutumika katika sekta hiyo.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa akisaini makubaliano na Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera ,Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Mkuu wa Taasisi ya DIT, Profesa Preksedis Ndomba amesema sekta ya viwanda inahitaji watu wenye ujuzi hivyo Taasisi ya DIT itakwenda na kasi ya kufua vijana wenye kwenye mafunzo mbalimbali.

Profesa Ndomba amesema kuwa makubaliano ni kwa ajili ya kuwapa mafunzo vijana 1000 katika chuo cha DIT Mwanza katika utengenezaji wa bidhaa za ngozi kutokana na Tanzania kuwa na mifugo mingi Afrika hivyo vijana watazalishwa na kuweza kujiajiri au kuajiriwa katika sekta ya ngozi.

Amesema DIT itakuwa bega kwa bega na serikali katika kuwaandaa katika sekta ya viwanda wakiwa na ujuzi ambao utawezesha viwanda hivyo viweze kukua katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.

Nae Mkurugenzi wa Ajira wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera ,Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Ally Msaki amesema makubaliano hayo yatakuwa endelevu kutokana na nia ya serikali katika kufikia vijana kuwa na ujuzi ambao unaweza kutumika na taifa likapata maendeleo.

Amesema katika utafiti uliofanywa na hiyo pamoja na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, inaonyesha kuwa watu walioko katika soko la ajira wanaujuzi mdogo.

Msaki amesema katika uandaji huo ni pamoja na VETA kuwa na mafunzo mbalimbali ya kutambua watu wenye ujuzi na kuwapa vyeti ili waweze kutambulika katika kufanya shughuli zao.

Aliongeza kuwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 serikali imetenga bilioni 15 kwa ajili ya kutolea mafunzo kwa vijana ili waweze kuwa sehemu soko la ajira.

Comments