Friday, January 20, 2017

Kuapishwa kwa Trump Kuwa Rais wa Marekani

trump

WASHNGTON DC, MAREKANI: RAIS Mteule wa Marekani, Donald Trump anataraiwa kuapishwa kuwa rais wa 45 wa nchi hiyo muda mfupi ujao majira ya saa 5:30 asubuhi kwa saa za Amerika ya Kaskazini sawa na saa 1:30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
trump-7
Trump anatarajiwa kuapishwa mbele ya watu 750,000 kwenye majengo Makuu ya Bunge la Marekani, Capitol Building, Washington D.C. Mnamo majira ya saa 2:30 asubuhi kwa saa za Amerika ya Kaskazini, ameondoka kwenye jeno la Blair na kuhudhuria misa akiambatana na mkewe Melania Trump na familia yao, katika Kanisa la St. John’s Episcopal.
trumpSaa 11:45 jioni hii (Saa 3:45 asubuhi kwa saa za Amerika ya Kaskazini);Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump sasa anaelekea Ikulu ya nchi hiyo (hite House) kama ratiba ya kuapishwa kwake inavyomtaka.
trump2
Saa 11:45 jioni hii (Saa 3:45 asubuhi kwa saa za Amerika ya Kaskazini);Tayari rais Barack Obama na mkewe Michele wamempokea Rais Mteule Donald  Trump na mkewe Melania, White House. Ataapishwa rasmi majira ya saa 1:30 jioni hii.
trump3
Tayari rais Obama amekwishaondoka Ikulu ya nchi hiyo huku akiwaaga Wamarekani na kuwashukuru watu wote wa nchi hiyo.
trump4  trump6trump8trump9trump10trump11trump12trump13trump14trump15trump16trump17trump18trump19trump20trump21
Post a Comment