Monday, May 12, 2014

MUAKILISHI WA JIMBO LA KWAMTIPURA AHUTUBIA WANACCM JIMBONI KWAKE

DSC_0217Muakilishi wa Jimbo la Kwamtipura Hamza Hassan Juma akiwahutubia wanachama wa CCM pamoja na wananchi mbalimbali katika Mkutano wa hadhara kuhusiana na Mchakato wa Bunge la katiba huko katika jimbo la kwamtipura Zanzibar.DSC_0231Wanachama wa CCM wakishangilia na kuonesha ishara ya vidole viwili wakimaanisha Serikali Mbili wakati wa Mkutano uliohutubiwa na Muakilmishi wa Jimbo la Kwamtipura Hamza Hassan Juma huko katika Uwanja wa mpira wa Mkele Zanzibar.DSC_0236Muakilishi wa Kwamtipura Hamza Hassan Juma akisoma baadhi ya Vifungu vilivyo muhimu kutoka katika Rasimu ya katiba alipowahutubia Wananchi na wana CCM wa Jimbo la Kwamtipura Zanzibar.DSC_0246Muakilishi wa Kwamtipura Hamza Hassan Juma akipeana mikono na wananchi na viongozi wa CCM waJimbo la Kwamtipura baada ya kumaliza mkutano wake wa hadhara Mkele Zanzibar. 
PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

BENKI YA EXIM YAISAIDIA WODI YA WAZAZI YA HOSPITALI YA RUFAA YA MWANANYAMALA

MWN PIX 1Meneja Msaidizi Masoko wa Benki ya Exim Tanzania, Bi Anita Goshashy (Watatu Kushoto) akikabidhi magodoro kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, Dkt. Sophinias Ngonyani (Kushoto). Wakishuhudia ni Wafanyakazi wa Benki ya Exim.  Benki ya Exim imetoa magodoro 60 katika Wadi ya Wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika kuadhimisha Siku ya Mama Duniani. Picha na Mpiga Picha Wetu. MWN PIX 4MWN PIX 5Meneja Msaidizi Masoko wa Benki ya Exim Tanzania, Bi Anita Goshashy (Watatu Kushoto) akikabidhi magodoro kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, Dkt. Sophinias Ngonyani (Kushoto). Wakishuhudia ni Wafanyakazi wa Benki ya Exim.  Benki ya Exim imetoa magodoro 60 katika Wadi ya Wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika kuadhimisha Siku ya Mama Duniani. Wa kwanza kushoto ni Muuguzi Kiongozi Sr. Tuswege Mwamwaja na Kulia ni Muuguzi Mkunga Bi. Marietha Mwageni. (Picha na Mpiga Picha Wetu)MWN PIX 6Meneja Msaidizi Masoko wa Benki ya Exim Tanzania, Bi Anita Goshashy (Wakwanza Kushoto)  na Meneja Msaidizi Msoko mwenzake Bi Violet Bikoche (Wapili Kushoto) wakizungumza na mmoja kati ya kinamama waliojifungua mara baada ya kukabidhi magodoro katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala.  Benki ya Exim imetoa magodoro 60 katika Wodi ya Wazazi Hospitalini hapo mwishoni mwa wiki katika kuadhimisha Siku ya Mama Duniani. (Picha na Mpiga Picha Wetu).MWN PIX 7Muuguzi Kiongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala Sr. Tuswege Mwamwaja (wa kwanza kulia) akifafanua jambo kwa wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania mara baada ya Benki hiyo kukabidhi magodoro 60 katika Wodi ya Wazazi Hospitalini hapo mwishoni mwa wiki katika kuadhimisha Siku ya Mama Duniani. (Picha na Mpiga Picha Wetu). MWN PIX 8Katibu wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Bi. Erica Mbutu (wakwanza kushoto) na Meneja Msaidizi Msoko wa Benki ya Exim, Bi Violet Bikoche (Wapili Kushoto) wakizungumza na mmoja kati ya kinamama waliojifungua mara baada ya kukabidhi magodoro katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala.  Benki ya Exim imetoa magodoro 60 katika Wodi ya Wazazi Hospitalini hapo mwishoni mwa wiki katika kuadhimisha Siku ya Mama Duniani. (Picha na Mpiga Picha Wetu).MWN PIX 9Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala Dkt. Sophinias Ngonyani (wa kwanza kulia) akifafanua jambo kwa wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania mara baada ya Benki hiyo kukabidhi magodoro 60 katika Wodi ya Wazazi Hospitalini hapo mwishoni mwa wiki katika kuadhimisha Siku ya Mama Duniani. (Picha na Mpiga Picha Wetu).
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya Exim ya Tanzania imeadhimisha Sikukuu ya Mama Duniani kwa kuchangia magodoro 60 katika wodi ya wazazi ya Hospitali ya Mwananyamala iliyopo jijini Dar es Salaam katika kutoa heshima kwa kinamama wote na kuunga mkono jitihada za kuboresha afya ya uzazi nchini. 
Kwa sasa, Hospitali ya Mwananyamala ambayo ni hospitali kubwa ya rufaa jijini Dar es Salaam inatoa huduma kwa wakinamama wanaotarajia kujifungua zaidi ya 3100 kwa mwezi, ikiwa na vitanda 136 tu katika wodi hiyo ya wazazi.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi magodoro hayo hospitali hapo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Meneja Msaidizi Masoko Bi Anita Goshashy alisema mchango huo ni moja kati ya utekelezaji wa shughuli za benki yake zinazolenga kuisaidia jamii inayoizunguka.
 “Mwaka jana, Benki ya Exim imeweza kufikia faida ya shilingi bilioni 20, na tumekuwa na utamaduni wa kurejesha kile tukipatacho toka kwa jamii. Sasa, leo hii tuko hapa Mwananyamala kukabidhi vitu hivi, ikiwa kama njia ya kutambua mchango wa kina mama zetu na kuonyesha jinsi gani tunaisaidia jamii inayotuzunguka kama benki,” alisema Bi. Goshashy, aliongeza kuwa benki itaendelea kuipiga jeki jamii hususani katika sekta ya Afya, Mazingira na Elimu.
Bi. Goshashy alisisitiza kuwa, “Leo hii tunakabidhi magodoro haya ili kuweza kusaidia kuboresha uzazi uliosalama. Kina mama wengi wanaotarajia kujigfungua ufariki wakati wakijifungua. Mchango wetu leo utasaidia katika katika kuboresha hali hiyo hapa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala. Jitihada zetu hazitaishia hapa tutaendelea kufanyakazi karibu na jamii inayotuzunguka.”
Naye Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Dkt. Sophinias Ngonyani aliipongeza Benki ya Exim kwa msaada huo, na kuongeza kuwa msaada umewafikia kwa wakati muafaka na kuziasa taasisi nyingine za kifedha na makampuni mengine nchini kuiga mfano huo.
“Kwa niaba ya Jamii ya Hospitali ya Mwananyamala, Ningependa kuelezea shukrani zangu za dhati kwa hatua nzuri mliyoichukua kuweza kutusaidia vitanda hivi ambavyo vitatumika kwa wakinamama ambao tunawathamini kwa kiasi kikubwa maishani mwetu. Mchango huu utasaidia Jamii ya Mwananyamala kwa kiaasi kikubwa  sana,” alisema Dkt. Ngonyani.
Dkt Ngonyani alisema kuwa kadri ya serikali inapojitahidi kuzipatia vifaa vituo vya afya, jitihada haziwezi kutoshereza mahitaji yote kwa ujumla katika hospitali hizi, ndiyo maana kuna haja ya wadau wengine, hususani makampuni kujitokeza na kuunga mkono jitihada hizo na kuweza kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya afya nchini.
“Nawapongeza kwa utekelezaji wenu mzuri wa sera yenu ya kufanya shughuli za kijamii. Ombi langu kwa benki ni kwamba bado tunakumbana na changamoto nyingi kama hospitali ya rufaa, Nawaasa msichoke kutupatia michango yenu katika sekta hii nyeti iokoayo maisha ya watu wetu,” Dkt. Ngonyani aliongeza.

Serikali yapokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Balozi wa Malawi hapa nchini Hayati Mhe. Flossie Gomile Chidyaonga

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa John M. Haule akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Juu ya Kifo cha aliyekuwa Balozi wa Mwalawi nchini Tanzania Hayati Mhe. Flossie Chidyaonga kilichotokea kwenye Hospitali ya Aga Khan Jijini Dar es Salaam siku ya Ijumaa Tarehe 09 Mei 2014.
 Bwa. John M. Haule akiendelea kuzungumza huku Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Vicent Kibwana (kushoto) akiyafuatilia kwa makini mazungumzo hayo na waandishi wa Habari (hawapo pichani)
 Mazungumzo yakiendelea kati ya waandishi wa habari na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.Picha na Reginald Philip
--  
 JAMHURI YA MUUGANO WA TANZANIA
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Serikali  imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Balozi wa Malawi hapa nchini Hayati Mhe. Flossie Gomile Chidyaonga kilichotokea Ijumaa tarehe 09 Mei, 2014. Balozi Chidyaonga alifariki akiwa njiani kupelekwa hospitali ya Aga Khan ya hapa Dar es Salaam.

 Balozi Flossie Chidyaonga alizaliwa tarehe 16 Juni, 1960 huko Blantyre nchini Malawi. Balozi Chidyaonga aliitumikia Serikali ya Malawi katika nyadhifa mbalimbali.  Kati ya mwaka 2006 hadi 2010 alikuwa Naibu Balozi wa Malawi nchini Uingereza na baadaye Kaimu Balozi hadi alipoteuliwa kuwa Balozi wa Malawi hapa Tanzanaia.

Siku ya Jumatatu, tarehe 05 Mei, 2014, Balozi Flossie Chidyaonga alishinda vizuri na kufanya shughuli zake kama kawaida. Hata hivyo, ilipofika usiku,  alijisikia vibaya na kupelekwa hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam ambapo alipatiwa Matibabu na kuwekwa mapunziko kuanzia saa 6 usiku hadi saa 12 asubuhi aliporuhusiwa na kupewa dawa za kutumia nyumbani. Balozi Chidyaonga aliendelea kutumia dawa hizo na hali kuonekana kuimarika hadi siku hiyo ya ijumaa, tarehe 09 Mei, 2014. Siku hiyo, aliamka vizuri hadi ilipofika majira ya saa 6 mchana, hali yake ilipobadilika na kukimbizwa tena hospitali ya Aga Khan ambapo alipokelewa Daktari alisema amekwishafariki. 
 
Sasa hivi, Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Uchunguzi wa madaktari umeonesha kuwa marehemu amefariki kutokana na Mshipa Mkuu wa AORTA kuvimba na kupasuka kulikosababisha damu kukusanyika kwenye mfuko wa moyo na hivyo kufanya moyo ushindwe kufanya kazi yake.

Kesho tarehe 12 Mei, 2014 mwili wa Marehemu utachukuliwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kupelekwa kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere ambapo kutafanyika misa ya kumuombea Marehemu na kutoa heshima za mwisho kuanzia saa 4 asubuhi. Mwili wa Marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwenda Blantyre, Malawi siku ya Jumanne tarehe 13 Mei, 2014 na mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumatano tarehe 14 Mei 2014 huko Blantyer, Malawi.

Katika kipindi chote alichokuwa mwakilishi wa Malawi hapa nchini, Balozi Chidyaonga alifanya kazi yake ya kukuza na kuendeleza ushirikiano kati ya nchi zetu mbili kwa umahiri wa hali ya juu. Siku zote alikuwa mstari wa mbele kutoa ushirikiano kwa Serikali na Mabalozi wenzake wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania.

Mungu aiweke roho ya marehemu Balozi Flossie Chidyaonga, mahali pema peponi.

AMEN

Imetolewa na 
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
 Dar Es Salaam, 
Tarehe 11 Mei, 201

Rais Jakaya Kikwete Atembelea Kiwanda Kikubwa Zaidi cha Saruji Duniani Dangote Cement Obajana Plant na kinachomilikiwa na tajiri mkubwa zaidi wa Afrika, Bwana Aliko Dangote


 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote katika uwanja wa ndege wa kiwanda chake cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela May 9, 2014. Kushoto ni Balozi wa Nigeria nchini Tanzania Mhe. Dkt. Ishaya Samaila Majanbu
 Rais Dkt Jakaya Mrisho kikwete akipata maelezo toka kwa mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote  wakati akizungushwa kuangalia kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela May 9, 2014
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa na  mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote kujionea maeneo mbalimbali ya kiwanda  cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela May 9, 2014. Kushoto ni Balozi wa Nigeria nchini Tanzania Mhe. Dkt. Ishaya Samaila Majanbu
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa na  mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote kujionea maeneo mbalimbali ya kiwanda  cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela May 9, 2014. Kushoto ni Balozi wa Nigeria nchini Tanzania Mhe. Dkt. Ishaya Samaila Majanbu

Soma Taarifa Ya Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT Tanzania) Kuhusu Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali katika taarifa yake ya mwaka 2012/2013

1. Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT Tanzania) kimesononeshwa sana na hoja za ukaguzi zilizoibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali katika taarifa yake ya mwaka 2012/2013. Taarifa ya CAG inaonyesha kuwa fedha za umma katika mwaka wa fedha uliotajwa zilitumiwa vibaya na watu waliokabidhiwa mamlaka ya kuzitunza na kuzitumia kwa ajili ya wananchi. 
Taarifa inaonyesha, kwa mfano, kwamba fedha za walipa kodi shilingi bilioni 1.6 ziliibwa kwa kulipa watumishi hewa waliokwishafariki dunia. Aidha, taarifa hiyo inaonyesha kuwa magari 11 ya Wizara ya Viwanda na Biashara yalitoweka katika mazingira tatanishi na hadi leo hayajulikani yalipo. Kwa kifupi, magari haya yamekwepuliwa na wajanja. 

2. Fedha hizi zimefujwa katika nchi ambayo zaidi ya theluthi ya watu wake wanaishi katika ufukara wa kutupwa, elimu inayozidi kuporomoka mwaka hadi mwaka, watu wanaopeteza maisha yao kwa magonjwa yanayotibika kutokana na huduma mbaya sana za afya, zaidi ya asilimia 90 hawana hifadhi ya jamii, zaidi ya nusu ya wananchi hawana maji safi na salama na miundombinu inayosombwa na maji kila mvua zikinyesha. Kwa hakika inatia hasira kuona matumizi ya hovyo ya fedha za walipa kodi tena bila hatua stahiki kuchukuliwa na watu waliokabidhiwa mamlaka na wananchi haohao wanaoteseka na wanaowaibia. 

3. Aidha, ACT Tanzania inachukizwa kuona kuwa maendeleo ya nchi yanachangiwa na wafanyabiashara wadogo, wafanyakazi na wafadhili ilhali wafanyabiashara wakubwa na wawekezaji wanapata ruzuku na serikali kupitia misamaha ya kodi yenye thamani ya shilingi 1.5 trilioni. 

4. ACT-Tanzania imekokotoa hoja za ukaguzi na kukuta kwamba kwenye masuala ya Serikali kuu pekee thamani ya hoja ni shilingi bilioni 867 ikiwa ni fedha zilizopotea. Kiwango hiki cha fedha kingeweza kumaliza ukarabati wa bandari ya Dar Es salaam kwa kujenga gati mpya, au kuweza kujenga vyuo vya ufundi vya VETA katika kila wilaya nchini. 

5. ACT-Tanzania imekaribisha kwa mikono miwili taarifa ya kwanza ya ukaguzi wa vyama vya siasa nchini. Hii ni historia ya kuenzi katika ujenzi wa jamii ya uwajibikaji. ACT-Tanzania inatoa rai kwa CAG kuweka wazi mahesabu ya kila chama ili wanachama wa vyama hivyo wajue namna vyama vyao vinavyoendeshwa. Vilevile ACT-Tanzania inamtaka CAG atoe Maelezo ya kina ni Kwanini hajakagua hesabu za chama cha CCM, lini atakagua na lini ataweka wazi mahesabu yao. 

6. ACT Tanzania imesikitishwa na Taarifa ya awali ya CAG inayoonyesha kuwa hakuna hata chama kimoja cha siasa kilichowasilisha mahesabu yake ambacho kilifuata taratibu za kiuhasibu katika kuwasilisha taarifa yake, jambo ambalo linatia shaka juu ya mwenendo wa matumizi ya fedha za umma katika vyama hivyo. 

7. ACT Tanzania inawaomba wananchi waitafakari taarifa ya CAG na kujitathimini na kuchukua hatua stahiki kuipumzisha CCM katika chaguzi zijazo kwa kuwa serikali yake imethibitisha miaka nenda rudi kuwa haiwezi kutunza na/au kutumia fedha za umma kwa maendeleo ya nchi na wananchi wake. 

8. ACT-Tanzania inawahimiza wabunge wenye kuamini katika sera za mrengo wa kushoto na dhana ya uwajibikaji kutumia taarifa ya CAG kwa kina wakati wa mijadala ya Bajeti, na kukataa kupitisha Bajeti za wizara ambazo CAG ameainisha madudu. 

Pamoja na Salamu za ACT Tanzania. 
(Signed) 
Samson Mwigamba 
Katibu Mkuu ACT-Tanzania

* ACT Tanzania ni Chama cha Siasa kilichoundwa kwa kufuata misingi ya Demokrasia Jamii na chenye shabaha kuu ya kusimamia Mabadiliko na Uwazi.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akili nchini, Gilbert Buberwa amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Dengue

Waombolezaji wakimfariji Leticia Filbert, mke wa daktari bingwa wa Hospitali ya Temeke, marehemu Dk Gilbert Buberwa nyumbani kwake Kinyerezi, Dar es Salam jana. Picha na Salim Shao  
--
 Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akili nchini, Gilbert Buberwa amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa dengue.

Kifo cha Dk Buberwa kinafanya idadi ya watumishi wa afya waliofariki dunia kutokana na ugonjwa huo kufikia wawili baada ya muuguzi Hamida Likoti kufariki dunia wiki iliyopita.

Ugonjwa huo uliolipuka mkoani Dar es Salaam, umezua taharuki kwa wakazi wake kwa sababu hauna tiba na unasababishwa na mbu, Aedes Egyptae, anayeuma mchana na anayeweza kuzaliana katika majisafi yaliyotuama.

Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Primus Saidia alisema jana kuwa Dk Buberwa alifariki dunia saa saba usiku wa kuamkia jana akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).Kwa habari zaidi Bofya na Endelea....

MAJINA YA WANAFUNZIWA KIDATO CHA SITA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JKT

Jeshi la Kujenga Taifa

                       

NMB YATOA SOMO LA KUJENGA MITAJI, YAHIMIZA AKIBA YENYE MALENGO

  DODOMA. Benki ya NMB imewataka Watanzania kujenga utamaduni wa kuweka akiba kwa malengo na kufanya maamuzi sahihi ya uwekezaji ili kuimari...