Wednesday, March 11, 2026

WAZIRI KATAMBI MBELE YA KAMATI YA MAMBO YA NJE ULINZI NA USALAMA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amewasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Miradi inayotekelezwa na Vyombo vya Usalama vilivyo chini ya wizara yake mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

Uwasilishaji huo umefanyika leo jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa kamati hiyo kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa miradi iliyotengewa fedha na Serikali kwa lengo la kuhakikisha uwajibikaji, ufanisi na thamani ya fedha katika matumizi ya rasilimali za umma.

Katika taarifa yake, Waziri Katambi alieleza hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na maendeleo ya miundombinu, ununuzi wa vifaa, pamoja na maboresho yanayolenga kuimarisha utendaji wa vyombo vya usalama nchini. 

Aidha, alifafanua namna ambavyo wizara inaendelea kusimamia utekelezaji huo ili kuendana na malengo ya Serikali ya kuimarisha amani, usalama na ustawi wa taifa.

Kamati ilipokea na kujadili taarifa hiyo kwa lengo la kupata ufafanuzi wa kina kuhusu maendeleo ya miradi, changamoto zilizojitokeza pamoja na mikakati ya kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyotarajiwa.







No comments:

Makamu wa Rais Dkt. Nchimbi Aungana na Waombolezaji Chato Katika Ibada ya Kumuaga Mama wa Hayati Dkt. John Magufuli

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa na waombolezaji mbalimbali kushiriki Ibada ya kumu...