Mkurugenzi wa kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa Suhail Esmail Thakore akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya mafanikio ya sekta ya viwanda yanavyozidi kukua na kumpongeza Rais wa awamu ya tano Dr John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuinua sekta viwanda hapa nchini.
Mkurugenzi wa kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa Suhail Esmail Thakore akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya mafanikio ya sekta ya viwanda yanavyozidi kukua na kumpongeza Rais wa awamu ya tano Dr John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuinua sekta viwanda hapa nchini.
Mkurugenzi wa kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa Suhail Esmail Thakore akiwa na waandishi wa habari wa mkaoni Iringa wakitembelea maeneo ya kiwanda cha Ivori Iringa
Mkurugenzi wa kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa Suhail Esmail Thakore akiongea na waandishi wa habari katika jengo jimpya ambalo litafunguliwa kiwanda kipya hivi karibuni
Mkurugenzi wa kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa Suhail Esmail Thakore akiwa kwenye picha ya pamoja na waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa pamoja na mdau wa chama cha mapinduzi (CCM) Hamza Ginga.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
KAMPUNI ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa imempongeza Rais Dk John Magufuli kwa namna alivyolipatia ufumbuzi suala la sukari ya viwandani ikisema litanusuru viwanda vilivyotaka kufungwa kutokana na uhaba wa bidhaa hiyo.
Katika Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, Machi 19, pamoja na mambo mengine yanayohusu sukari, Rais Magufuli alisema hakuna sababu kwa taifa kutumia fedha nyingi za kigeni kuagiza sukari toka nje ya nchi wakati uwezo wa wafanyabishara kuzalisha sukari hiyo nchini upo.
Dk Magufuli alisema mahitaji ya sukari nchini ni tani 590,000 kwa mwaka, ambapo tani 455,000 ni kwa ajili ya matumizi ya majumbani na tani 135,000 kwa ajili ya viwandani.
Alisema kwasasa kuna upungufu wa tani 125,000 za sukari ya kutumia majumbani na tani 135,000 kwa ajili ya matumizi ya viwandani.
Akizungumza na wanahabari wakati akielezea mafanikio na changamoto uzalishaji katika viwanda hivyo, mkurugenzi wa kampuni hizo, Suhail Esmail Thakore alisema wamepokea kwa furaha kubwa uamuzi wa serikali wa kushughulikia upungufu huo.
“Namshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuchukua hatua ya haraka sana kushughulikia tatizo la sukari. Taarifa tuliyopata mara baada ya kikao kile ni kwamba taratibu za kupata vibali vya kuagiza sukari ya viwandani kwa kuzingatia mahitaji ya viwanda vyetu zinaendelea. Hiiimetupa uhakika wa kuendelea na uzalishaji,”alisema.
Alisema viwanda vyake viliingiwa na hofu ya kusimamisha uzalishaji baada ya serikali kuzuia uagizaji wa sukari hiyo toka Novemba mwaka jana.
“Viwanda vyetu vivyoatumia malighafi zinazozalishwa na wakulima wa ndani ya nchi, zinazalisha bidhaa mbalimbali zinazojulikana kwa jina la Ivori zikiwemo tomato na chill sauce, pipi, chocolate na unga wa cocoa,” alisema.
Katika kipindi cha miaka michache iliyopita, Thakore alisema kumekuwepo na ongezeko la matumizi ya bidhaa hizo ndani ya nchi, na zinahitajika sana katika nchi jirani za Kenya, Kongo, Rwanda na Burundi hali inayowasukuma kuongeza uwekezaji ili kuunga mkono azma ya Rais ya Tanzania ya Viwanda.
Thakore alisema kwasasa viwanda vyao vinazalisha asilimia 30 tu ya mahitaji yao yote ya soko na katika kukabiliana na changamoto hiyo wameanza na ujenzi wa kiwanda kipya cha pipi kitakachowawezesha kufikia hadi asilimia 50 ya soko.
“Tunatarajia kufungua kiwanda hicho kipya kati ya mwezi Juni na Julai mwaka huu. Na mwaka 2019/2020 tutaanza ujenzi wa kiwanda kingine kikubwa cha kuzalisha bidhaa hizo hatua itakayotuwezesha kukaribia mahitaji ya soko letu,” alisema.
Akitoa mfano wa mahitaji ya soko la nje ya nchi, mfanyabishara huyo alisema walitakiwa na wafanyabiashara wa Burundi kusambaza tani 30 za bidhaa hizo kila mwezi lakini wanashidwa kufikia kiwango hicho kwasababu uzalishaji wa sasa hauwawezeshi kufanya hivyo.
Akizungumzia mahitaji ya sukari kwa ajili ya viwanda vyao alisema, wanahitaji zaidi ya tani 1,600 kwa ajili ya kiwanda cha Ivori Ltd na tani zaidi ya 1,500 kwa ajili ya kiwanda cha Iringa Food and Bevarage.
“Hata hivyo mahitaji hayo yataongezeka mara mbili zaidi kutokana na upanuzi wa kiwanda tunaofanya. Kwahiyo tutaiomba serikali itusaidie kupata sukari hiyo ili kukidhi mahitaji ya viwanda vyote na upanuzi wake,” alisema.
Thakore alitoa wito kwa watanzania kujiwekea kipaumbele cha kutumia bidhaa za ndani ili kuinua maendeleo ya viwanda, na kuongeza ajira na mapato ya wadau na Taifa.
Comments